Makala Ya Wazi: Kuchanganya Dini Na Siasa Kutaligharimu Taifa

Profesa mmoja wa sayansi ya siasa aliandika chapisho muhimu kuhusu Tanzania, ambapo pamoja na mambo mengine alieleza upekee wa nchi yetu kuwa yenye amani kubwa licha ya kuwa na takriban recipes nyingi za kufanya taifa liwe kwenye conflict.

Moja na ya recipes hizo ni tofauti kubwa ya kipato sio tu kati wenye nacho na wasio nacho bali pia kati ya dini kuu nchini Tanzania, yaani Wakristo na Waislamu.

Tofauti hiyo imechangiwa pia na “ukosefu wa usawa” kielimu na ajira kati ya dini hizo mbili.

Na kwa vile licha ya mchango wao mkubwa kwenye mapambano ya kudai uhuru kutoka kwa mkoloni, Waislamu wengi Tanzania wamekuwa na hisia za mfumo unaowabagua katika nyanja za elimu na ajira, manung’uniko yaliyoanza kujitokeza waziwazi baada ya serikali “kuianzisha” BAKWATA baada ya “kuifukuza” EAMWS in 1960s yameendelea kuwepo hadi sasa. Mbinu inayotumika kuyazima manung’uniko hayo ni kudhibiti mjadala wowote kuhusu hilo, sambamba na kile kinachotafsiriwa na baadhi ya Waislamu kuwa BAKWATA ni tawi la CCM/Serikali.

Kwahiyo, manung’uniko ya kundi moja kubwa la kidini + pengo kubwa kati ya wenye nacho na wasio nacho, jumlisha na factors kama massive youth unemployment, bila kusahau jitahidi endelevu za “kumwaga sumu kwenye kisuma” kwa kuendeleza siasa za chuki, ni dhahiri kuwa kuna mtu aidha amechoka kuiona Tanzania ikiendelea kuwa na amani au ni wakala wa nchi ya kigeni inayotamani kuiona Tanzania ikiteketea.

Goes like this, leo viongozi wa makanisa na misikiti wakifanikiwa kutumika kuwabagua wafuasi wa vyama vya upinzani basi si ajabu kesho wakijituma kubaguana kati ya Wakristo na Waislamu. Kama alivyotuusia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuhusu ubaguzi

Unadhani nini kifanyike kukabiliana na haya yanayoendelea? Niandikie HAPA

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali