Makala Ya Wazi: Kijarida Cha #MtuHatari

Mie mtumishi wako nafahamu fika kuwa kuna watu wengi tu wasiopendezwa na matangazo mbalimbali ninayowatumia. Na ndio maana kila ninapowatumia matangazo huwa nawaomba radhi, hasa kwa vile ukurasa huu ni wenu na mie ni mtumishi wenu tu.

Kabla ya kuingia kwenye makala ya wazi ya kijarida cha #MtuHatari kinachotumwa kila Jumapili kwa wanachama wa vijarida vya #BaruaYaChahali (unaweza kujiunga kwa KUBONYEZA HAPA) naomba niwasumbue na tangazo linalohusiana na lengo la kijarida cha #MtuHatari: kukufanya uwe mtu bora na/au kunoresha ubora wako.

Kitabu hiki kipya cha kielektroniki ni sehemu ya kwanza ya mlolongo wa vitabu (series) kuhusu “Jinsi Ya Kuwa Mtu Bora Au Kuboresha Ubora Wako.”

Mada husika ni hii:

Wanasema "vitu vizuri kula na wenzako." Na ndio maana wengine tunajihangaisha kushea nanyi japo kidogo tunachofahamu.

Mtu anaweza kukupa mamilioni ya shilingi lakini yakaisha, aidha kwa matumizi ya kawaida au kuibiwa au kudhulumiwa. Lakini mtu akikupa mbinu/ujuzi/uelewa, hubaki nawe milele unless uamue kupuuza. Na hakuna jambazi wala tapeli wa kukupora mbinu/ujuzi/uelewa.

Na ndio maana kesho nakuletea kitabu cha kielektroniki (ebook) cha kukusaidia kuwa mtu bora au kuboresha ubora wako. Ni mada 50 za kukupa mwongozo mwepesi kwa lugha rahisi kueleweka
.
Wanasema "msomi ni mtu anayeweza kueleza mambo magumu kwa lugha nyepesi," na ndivyo nifanyavyo mtumishi wako #EvaristChahali.

Enewei, lengo la mada hii ya jioni ni hiyo video hapo juu. Kila mara nafasi inaponiruhusu huwa ninafanya kitu kinachofahamika kama ECOTHERAPY au kwa jina jingine NATURE THERAPY au GREEN THERAPY

Kiambishi awali (prefix) "ECO-" kinaashiria "inayohusu asili/mazingira." Mfano ECOlogy" ni somo linalohusu asili (nature)/mazingira
.
"Therapy" maana yake "tiba." Kwahiyo "ecotheraphy" ni "tiba inayotokana na asili/mazingira." Na mazingira ni pamoja na uoto wa asili - misitu, mapori, nk, mito/maziwa/bahari, milima, nk

Japo neno therapy ni tiba, na tiba huhusishwa na maradhi, lakini ecotherapy si lazima itumiwe na wanaohitaji tiba kwa sababu ya maradhi.

Labda nikupe mfano unaonihusu. Mie ni mtu ninayependa kuongeza uelewa wangu kila siku. Kila siku lazima nijifunze kitu kimoja au zaidi. Kama sio mtandaoni basi kitabuni au katika maongezi na watu mbalimbali.

Lakini huku kujaza vitu vingi kichwani kunauchosha ubongo, na pasipo kuupatia mapumziko, inaweza kusababisha uchizi.

Ndio maana kila nafasi inaponiruhusu huwa nafanya hii ecotherapy, nakwenda sehemu iliyotulia na kukaa hapo kwa muda nitakaoona unafaa (yaweza kuwa nusu saa au masaa kadhaa)
.
Hapa Glasgow kuna kijimto (canal) kimoja kirefu kinapita sehemu mbalimbali za jiji hili, kinaitwa Forth & Clyde Canal. Pembeni mwake ni njia kwa ajili ya waendesha baiskeli na watembea kwa mguu. Na canal hiyo inatoa fursa mwafaka kwa ajili ya ecotherapy.

Unaonaje kuanzia mwezi mpya wa Septemba hapo kesho nawe ukaanza hii ecotherapy?

Nakutakia heri ya mwezi mpya wa Septemba

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali