Makala Ya Wazi: Kabudi Anaweza Kumzamisha Jiwe

Kwanza naomba niwafahamishe wale wote ambao msingependa niwasumbue kwa kuwatumia baruapepe mbalimbali, mnaweza kujiondoa kwa KUBONYEZA HAPA.

Kwa mtakaoamua kubaki/kutojiondoa, nitawawekea muhtasari hapa wa kila kijarida kilichotumwa kwa waliojiunga kuwa wanachama wa #BaruaYaChahali. Again, kama hutaki kutumiwa muhtasari huo, basi fanya kujiondoa (UNSUBSCRIBE)

Licha ya muhtasari wa vijarida, kutakuwa pia na “MAKALA ZA WAZI.” kama hii, ambazo zitakuwa “wazi” hata kwa msio wanachama.

Na makala ya kwanza katika mfululizo huo wa makala za wazi ni hii inayohusu jinsi mahojiano aliyofanyiwa Profesa Kabudi na BBC Swahili hapa Uingereza yalivyoweka wazi “siri” kuhusu kilichomkuta mwandishi wa habari AZORY GWANDA “aliyepotea” kwa zaidi ya mwaka sasa.

Na mara baada ya “kulikoroga,” watetezi mbalimbali wa uhuru wa habari duniani “wakalianzisha”

Hakuna kitu hatari kama mtu aliyeelimika anapogeuka “asslicker.” Na huyu mad professor anaelekea kuwa tayari kusema lolote lile kumpendeza Jiwe. Inatuumiza sana sie tunaothamini elimu, kwa sababu huyu profesa wa sheria ana kila sababu ya kusimamia uweledi wake kitaaluma, lakini kaamua kuwa mpambe wa Jiwe.

Kinachokera zaidi ni kuwa muongo bila kuona aibu. Tena anaongopa huku anaongea kwa kujiamini.

Lakini mara zote watu wenye uwezo wa japo kukemea maovu wanapoamua kuendekeza njaa zao na kuwa sehemu ya mfumo kandamizi, anguko dhidi ya mfumo huo halitowanusuru.

Kabudu sasa hivi ndio sura ya Jiwe huku nje, na huenda anapata jeuri ya “kulikoroga” kwa sababu at the end of the day, lawama zinaelekezwa kwa Jiwe na sio yeye “profesa msema chochote.”

Hatma ya nchi ya Tanzania sio nzuri. Leo kwa Azory, kesho kwako.

Naomba utumie muda wakutosha kutafakari kwa kina kuhusu kilichomsiba Azory. Tafakari kwa kina kuhusu mustakabali wa Tanzania yetu.

Naomba ruhusa kuhitimisha makala hii na tangazo hili hapa chini

Uanachama kwa mwaka mzima ni sh100,00 au sh 10,000 kwa mwezi. Tuma mchango wako kwa m-pesa namba 0767632516 (jina Khadija Katule). Kwa walio nje ya Tanzania, unaweza kuchangia kwa KUBONYEZA HAPA.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali