Makala Ya Wazi: Jitihada Mpya Za Kuondoa Ukomo Wa Urais

Jitihada za kumfanya Jiwe atawale milele zinaendelea. Na sasa zinaanza kuchukua mkondo wa kisheria/kikatiba. Hizi kelele sio za bahati mbaya, na kamwe usihadaiwe na porojo za Jiwe kuwa akimaliza muda wake ataondoka madarakani. He can’t kwa sababu once he does, ataelekea jela on the same day.

Patrick Dezydelius Mgoya, mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam amefungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania akihoji uhalali wa kifungu cha 40(2) cha katiba ya nchi, ambcho kinachotoa ukomo wa kipindi cha Urais. 

Katika kesi hiyo, Mgoya ameomba mahakama kutoa ufafanuzi wa kina na athari za kifungu hicho cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia ameiomba mahakama kutoa ufafanuzi sahihi wa kisheria na wa kina wa kifungu cha 42(2) cha katiba, na namna kinavyohusiana na vifungu namba 13, 21 na 22.

Kifungu namba 13 kinazungumzia usawa mbele ya sheria, namba 21 kinaelezea uhuru wa kushiriki shughuli za umma huku namba 22 kikielezea haki ya kufanya kazi.

Ameomba mahakama kutoa ufafanuzi wa kifungu namba 40(2) kwa pamoja na kifungu namba 39 ambacho kinaelezea sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais.

Katika hoja yake Mgoya amesema kuwa kwa kuweka ukomo wa kipindi cha Urais, kifungu 40(20) kinakiuka vipengele vingine vya katiba ambavyo vinatoa uhuru kwa wanachi kushirki katika shunguli za umma.

Hizi drama mtazielewa vizuri zaidibaada ya uchaguzi mkuuwa mwaka 2020. Unaweza kuhifadhi bandiko hili kwa kumbukumbu.

Nimalizie kwa tangazo la vitabu vyangu hivi viwili.

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali