Makala Ya Wazi: Dear Chadema, Hili La Uchaguzi Wenu Litawagharimu

Kukwepa Uchaguzi Ni Time Bomb, Litalipuka Muda Wowote Ule

Kwanza naomba kuwataka radhi wanachama wa #BaruaYaChahali kwa kuchelewa kuwatumia vijarida vya wiki hii. Ninaahidi kutekeleza jukumu hilo mapema iwezekanavyo.

Kwa muda mrefu nimekuwa miongoni mwa watu wanaoihamasisha Chadema kuhusu haja ya kufanya uchaguzi wa viongozi wa chama hicho. Na miongoni mwa hoja zangu ni kwamba Chadema inapaswa “kuishi kulingana na jina lake,” Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo. Sasa ni demokrasia gani hiyo ambapo Mbowe amekuwa kama Mwenyekiti wa kudumu?

Naam, Mbowe atabaki kuwa mmoja wa wanasiasa waliofanya mambo makubwa kabisa katika siasa za Tanzania. Mpende au mchukie, mwanasiasa huyu ni mmoja wa majabali wa siasa za nchi yetu. Na sina shaka hata chembe kuwa akisimama kwenye uchaguzi wa ndani Chadema dhidi ya mwanasiasa yeyote yule, atashinda kwa kishindo.

Sasa kwanini basi Chadema inaruhusu walakini huo wa kukwepa kufanya uchaguzi miaka nenda miaka rudi? Hoja kwamba Mbowe ameifanyia mengi Chadema na hakuna haja ya uchaguzi ni fyongo.

Lakini tatizo hapa sio tu ufyongo wa hoja hiyo bali hatari inazoambatana nayo. Moja ya hatari hiyo ni taswira hasi kuwa “neno Demokrasia” kwenye jina la chama hicho ji magumashi tu, maana demokrasia ni pamoja na kuchagua viongozi wapya kila baada ya muda flani (na by “wapya” haimaanishi kuwa wale waliopo madarakani hawapaswi kuchaguliwa tena unless Katiba inawazuwia).

Hatari nyingine ni kuwapa MATAGA cha kuongea. Moja ya “tusi” maarufu la MATAGA kwa Chadema ni hilo la “ufalme wa Mbowe.” Na kwa bahati mbaya, mara nyingi utetezi wa wana-Chadema huishia kuonekana usio na mashiko.

Lakini hatari kubwa zaidi ni hizi zama hatari za Jiwe ambapo ameshaonyesha bayana kuwa ana chuki kubwa mno dhidi ya upinzani na viongozi wake. Na sidhani kama Chadema hawaelewi how far Jiwe could go kwa minajili ya kuuangamiza upinzani.

Sasa kama Chadema wanamjua vema Jiwe na jinsi anavyotafuta kila mbinu kuua upinzani, kwanini basi wamrahisishie kwa kukiuka kanuni zao wenyewe kuhusu uchaguzi wa viongozi wa chama hicho kila baada ya muda flani?

Na baadhi yetu tulishajua mapema kuwa ji suala la muda tu kabla Jiwe kwa kupitia watendaji wake hajaishukia Chadema kama mwewe kwa kigezo cha kukiuka “taratibu za sheria ya vyama vya siasa inayotaka vyama hivyo kufanya chaguzi za ndani kila baada ya muda flani.”

And our worst fears have now been realised, kama inavyojitanabaisha kwenye barua hii

Sintoshangaa nikipokea mrejesho wa matusi kutoka kwa makada wa Chadema ambao ukitaka kukosana nao uliza au ongelea kuhusu uchaguzi wa ndani katika chama hicho.

Lakini pia sintoshangaa kusikia viongozi na wafuasi wa chama hicho wakijipa matumaini kuwa “hakuna mwenye uwezo wa kuifuta Chadema.”

Nachoweza kuwatahadharisha ni kwamba kama Ben Saanane “alipotezwa” baada ya kumkosoa Jiwe na hakuna lolote lililofanywa na Chadema dhidi ya mtuhumiwa namba moja wa “kupotea” kwa Ben, na kama Tundu Lissu alimwagiwa risasi lukuki kwa lengo la kumuua, nae kama Ben, baada ya kuwa mkosoaji maarufu wa Jiwe, na kana kwamba jaribio la kumuua halitoshi, Jiwe kampora Lissu ubunge, na kama Sugu alikwenda jela baada ya kumkosoa Jiwe na kama kawaida yao, Chadema walinywea, na kama Jiwe alimudu kumuweka ndani Lema na baadae Mbowe na Esther Matiko kwa miezi kadhaa, na hakukuwa na jitihada zozote kwa Chadema kupambana dhidi ya uhuni huo wa kisiasa, kwanini basi isiwezekane kwa Jiwe kutumia mwanya huu wa “Chadema kukiuka kanuni za vyama vya siasa kwa kutofanya chaguzi za ndani” na kukifuta chama hicho (God forbid)?

Naam twaomba Mungu aepushe hilo lisitokee lakini kwa kuzingatia hujuma mbalimbali za Jiwe dhidi ya Chadema “zilivyopokelewa kwa utiifu na chama hicho kikuu cha upinzani,” our worst fears might be realised again.

TANGAZO: Karibu kununua vitabu hivi endapo utahitaji

Pia unaweza kujiunga uanachama wa #BaruaYaChahali yenye vijarida vitano kwa wiki,  KWA KUBONYEZA HAPA (na kama unakerwa kutumiwa baruapepe kutoka kwangu,BONYEZA HAPA KUJIONDOA)

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali