Makala Ya Wazi: Achana Na VODA Kama Unajali Haki Yako Ya Faragha

Kumbuka Mabadiliko Huanza Na Mtu Mmoja.

Image

Moja ya mambo yanayokera mno kuhusu Tanzania yetu ni “ukondoo” wa wananchi. By “ukondoo” ninamaanisha watu wazima na akili zao kufanywa - ashakum si matusi - MAFALA. Badala ya kukasirika, watu wengi wapo bize na ubuyu, kubeti na vitu vingine visivyo na msingi.

Ukienda sehemu kama Instagram huwezi kuamini kuwa muda huu tunaoongea, kuna mamia kama sio maelfu ya watu “waliopotea” huko MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji), mpigania haki maarufu Tundu Lissu alimwagiwa risasi na kunusurika kufa lakini serikali imepuuzia japo kutuhadaa kuhusu wahusika, watu wanaendelea kutekwa kama zaha, Jiwe anamtumia Musiba kwachafua mamia ya Watanzania wasio na hatia, na matukio mengine kadha wa kadha.

Majuzi, mwandishi wa habari Eric Kabendera alitekwa na “Watu Wasiojulikana,” lakini kelele mfululizo zilipelekea polisi kuibuka na kudai anashikiliwa kwa makosa ya uhamiaji.

Kwa taarifa nilizonazo, Eric alitekwa kufuatia kifo cha afisa wa kitengo cha EU huko Hazina aliyeuawa majuzi. Taarifa zinadai kuwa afisa huyo alikuwa na taarifa nyeti kuhusu ufisadi mkubwa unaofanywa na Jiwe na mpwa wake pale Hazina, ufisadi unaohusisha kutafuna fedha zinazotolewa na EU. Taarifa kuwa kutekwa kwa Eric kunatokana na hisia ya Jiwe na watu wake kuhisi kuwa marehemu alimpatia Eric nyaraka zenye ushahidi wa ufisadi huo. Hapa ndipo ilipofikia Tanzania yetu.

Samahani kama nitaonekana kuwa kama “prophet of doom” (nabii wa majanga) lakini nadhani hali huko mbele itakuwa mbaya zaidi hasa kwa vile inaonekana kama watu wengi “wamekubali matokeo.”

Hata hivyo, sie tunaokerwa kwa dhati na mwelekeo wa taifa letu tunalazimika kutokaa kimya. Na nyie mlioamua kukaa kimya, mnaweza kuchukua hatua hii ndogo japo yenye nguvu kubwa, na uzuri ni kwamba ipo ndani ya uwezo wenu.

Tukio la kutekwa kwa Eric liliwezeshwa na Voda kuendeleza uhuni wao wa kuruhusu mawasiliano ya wateja wao kuchukuliwa na mamlaka. Utetezi wa kampuni hiyo ni wa kipuuzi

Image

Sasa ni fursa yako “kuwapiga finger” hawa wahuni. Kwa sababu kama wanaweza kufanya uhuni kwa watu maarufu zaidi yako, kwanini washindwe kufanya uhuni kwako?

Kwahiyo, wito wangu kwako ni kuachana na hawa wahuni, na sio kuachana nao tu, bali pia jitahidi kushawishi watu wengine kuachana na uhuni huu. Laiti kila mtu anayepokea ujumbe huu akiweza kushawishi japo watu 10, na hao 10 wakashawishi 10, muda si mrefu idadi inaweza kufikia hadi watu milioni. Lengo sio kuikomoa Voda bali kuiadhibu kwa kupuuzia haki za nyie wateja wake, ambao kimsingi ndio mnaiwezesha kampuni hiyo kuendelea na biashara.

Image

Na mkiiadhibu Voda basi makampuni mengine ya simu yataamka na kubaini kuwa Watanzania sio tena “kondoo” wa kupelekeshwa ovyo, kwamba sasa sio tu wanatambua haki zao bali pia wanachukua hatua pindi haki zao zinapochezewa.

Naomba nihitimishe kwa tangazo hili hapa chini (samahani kwa nitakaowakwaza)

TANGAZO: Jinsi ya kujiungana #BaruaYaChahali: Uanachama kwa mwaka mzima ni sh100,00 au sh 10,000 kwa mwezi. Tuma mchango wako kwa m-pesa namba 0767632516 (jina Khadija Katule). Kwa walio nje ya Tanzania, unaweza kuchangia kwa KUBONYEZA HAPA.

Endapo unataka kuondolewa kwenye orodha ya wanaotumiwa #BaruaYaChahali JIONDOE HAPA.

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali