Barua Ya Chahali
Jasusi
Mahojiano Na Dokta @ZakayoMmbaga: Jinsi Kuuguliwa Udogoni Kulivyompa Hamasa Ya Kuja Kuwa Daktari
0:00
-40:56

Mahojiano Na Dokta @ZakayoMmbaga: Jinsi Kuuguliwa Udogoni Kulivyompa Hamasa Ya Kuja Kuwa Daktari

Katika mahojiano haya, Dokta Zakayo Mmbaga anaeleza kuhusu 

👉 Jinsi kuuguliwa na nduguye kulivyomfanya atamani siku moja awe daktari, na hatimaye ikaja kuwa hivyo. 

👉 Jinsi kusaidia kuhudumia mifugo kulivyompa uzoefu wa kwanza wa kuchoma sindano na kutibu vidonda, na kumtamanisha zaidi kuja kuwa daktari. 

👉 Jinsi alivyorudi likizo na kukuta nduguye anaumwa kansa lakini ndugu wengine hawakufahamu na wakawa na matumiani kuwa mgonjwa atapona lakini yeye kama daktari mwanafunzi alifahamu kuwa mgonjwa huyo angefariki. Hata hivyo hakuweza kumwambia mtu yeyote, kitu ambacho kilimuumiza nafsini. 

👉 Jinsi gharama kubwa wanayoingia madaktari wanafunzi zinavyowafanya kuendelea kuwa na madeni yasiyolipika, huku jaribio la kujiendeleza kitaaluma likimaanisha madeni zaidi. 

👉 Jinsi mazingira magumu ya kazi yanavyofanya taaluma ya utabibu kuwa ngumu, hasa pale inapolazimika kumuelekeza mgonjwa aende hospitali ya rufaa ilhali uwezo wake kifedha ni mdogo. 

Kwa hakika mahojiano haya yanahamasisha, yanatafakarisha na yanasikitisha.

0 Comments