Magufuli Akosolewa Na Swahiba Yake Mkuu Raila Kuhusu Korona Tanzania

Kuna makala ya uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu suala la korona nchini Tanzania na mustakabali wa utawala wa Rais John Magufuli, na ninachoweza “kukuibia” msomaji ni mtazamo wangu kuwa “korona itaondoka na Magufuli” (si kwa maana ya gonjwa hilo kuchukua uhai wake -siwezi kumwombea mtu maambukizi ya ugonjwa huo hata awe adui yangu mkubwa — bali “uhai wa utawala wake.”)

Na miongoni mwa mambo niliyoongelea ni uwezekano mkubwa kwa Magufuli kutengwa na nchi jirani kwa sababu mzaha wake katika kushughulikia janga la korona una athari kwa majirani wa Tanzania pia. Endapo nchi hizo zitafanikiwa kudhibiti janga hilo, zitalazimika kuidhibiti Tanzania, kwa sababu kinyume chake watajikuta wanarudishwa nyuma.

Taarifa kutoka Uganda na Rwanda zinaeleza kuwa tayari kuna dalili za chuki dhidi ya Watanzania, hali inayoweza kusambaa kwa nchi nyingine majirani zetu.

Na pengine ishara kubwa zaidi ya “yajayo,” ni mahojiano haya aliyofanyiwa swahiba mkubwa wa Magufuli, mwanasiasa maarufu wa Kenya, Raila Odinga, ambaye bila kuuma maneno amemlaumu rafiki yake “kidiplomasia” kwa kusema “anashauriwa vibaya.”

Kwa upande mwingine, upuuzi alioongea Magufuli Jumapili kuhusu “papai liitwalo Elizabeti Anne”

na madudu mengine kama hayo, na hatimaye kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Maabara Kuu ya Serikali Dkt Nyambura Moremi,

tamko la Bashite kuwa wabunge wa Chadema walioji-isolate warudi Dodoma ndani ya masaa 24

na tangazo la Mtu Mfupi Ndugai kuwa Mwambe arejee Bungeni,

kwa pamoja ni jitihada za makusudi za serikali ya Magufuli kuwatoa relini, msitafakari kuhusu uhuni unaofanywa na serikali hiyo kwenye janga la korona, mbaki mnajadili upuuzi wao.

Unfortunately, it is working maana Watanzania kwa kudakia matukio hawajambo.

Enewei, chukua tahadhari dhidi ya korona, jikinge na uwakinge wenzio pia.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali