Madai Kuwa Bashite Alikuwa Dodoma Wakati Mbowe Anashambuliwa

Nimekutana na uzi mmoja wa mdau huko Jamii Forums kuhusu uwezekano kwamba Daudi Bashite anahusika na shambulio dhidi ya Mbowe

Leo Jumanne 09 Juni 2020, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, aliandaa Mkutano na Madereva Bodaboda. Sijajua alitaka kuongelea nini, lakini ni kwamba aliwakusanya Madereva wote Bodaboda maeneo ya Leaders Club Wilayani Kinondoni mkoani Dar Es Salaam kuanzaia Saa Mbili asubuhi.

Ilipofika Saa Sita na Nusu bado Mkuu wa Mkoa alikuwa hajafika, kitendo kilichofanya Madereva bodaboda kuanza kulalamika kwamba wanachelewa kwenda kufanya kazi. Akatokea mtu mmoja akaropoka kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda hatafika kwani yupo Makao Makuu ya Nchi.

Bodaboda kusikia hivyo walianza kutawanyika na kuelekea kwenye Vituo vyao vya kazi. Pamoja na kwamba MC wa Shughuli aliwasihi kurudi na kusubiri Mkuu wa Mkoa afike kwani huwezi jua kawaandalia nini, Waligoma katakata.

Hata hivyo, baada ya muda, yule Jamaa aliyetangaza kwamba Mkuu wa Mkoa hatafika Leaders Club, akakamatwa na Watu wanaodaiwa ni UVCCM wakamkabidhi kwa Polisi ambao walimkimbiza na kumpakia kwenye gari la Polisi.

Swali langu ni: Je, ni kweli Paul Makonda jana alienda Dodoma? Alienda kufanya nini?

Video:

<iframe src="

width="640" height="564" frameborder="0" allow="autoplay; fullscreen" allowfullscreen></iframe>

Tukiachana na tuhuma hizo za mdau, mimi binafsi ninaamini kuwa Magufuli na mwanae Bashite wanahusika kwa asilimia 100 katika unyama huu.

Na wala hakuhitajiki ushahidi kuthibitisha hilo.

NB: Kesho nitawasilisha uchambuzi kuhusu tamko la Lissu kuwania Urais na pia kuongelea kwa muktadha kuhusu shambulizi dhidi h Mbowe.

🙏