Maandamano ya kupingwa muswada wa fedha Kenya: muhtasari kuhusu hotuba za Ruto na Gachagua na mustakabali wao, hatma ya shushushu mkuu Noordin Haji
Kenya imekuwa ikikabiliwa na maandamano makubwa yanayotokana na Muswada wa Fedha wa 2024 unaopingwa kwa nguvu na sehemu kubwa ya wananchi. Maandamano haya yameongezeka hadi kufikia vurugu, zilizosababisha vifo na migogoro ya kisiasa.
Makala hii inahusu muhtasari wa matukio muhimu ya hivi karibuni yanayohusiana na maandamano, hotuba za Rais William Ruto, wito wa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa Noordin Haji kujiuzulu, na utata unaozunguka jibu lililotolewa na Haji.