Usiku wa manane wa tarehe 25 ya mwezi uliopita - yaani mwezi kamili sasa - Dokta Emmanuel Nchimbi akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivamiwa nyumbani kwake na kuwekwa chini ya ulinzi na maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Muda mfupi baadaye, maafisa hao waliondoka nae nae kuelekea kwenye jengo moja linalomilikiwa na idara ya Usalama wa taifa.
Kadhalika, usiku huohuo, maafisa wengine waliokuwa kwenye operesheni maalumu waliingia kwenye akaunti ya Instagram ya mwanasisasa huyo na kuandika ujumbe ulioleza kuwa Dkt Nchimbi anajiuzulu.
Na tangu wakati huo Dkt Nchimbi hajaonekana tena. Mara ya mwisho kuonekana na kusikika hadharani ilikuwa Agosti 22 katika uzinduzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere.
Makala hii inaeleza yaliyojiri baada ya Dkt Nchimbi kuwekwa kizuizini na kujibu swali linalowatatiza wengi endapo yupo hai au la.
Lakini kabla ya kuendelea na makala hii, Jasusi anapenda kuwafahamisha kuhusu kuchapishwa kwa kitabu maalum kuhusu sakata la Dokta Nchimbi, kikieleza siri zilizofichika nyuma ya kung'olewa madarakani kwa kiuongozi huyo.
Lengo hasa la kitabi huki ni kuweka rekodi ya tukio hilo muhimu hasa kwa vile Watanzania hawana utamaduni wa kuhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu.
Tuanze na yanayofahamika



