Kwa Minajili Ya Kumbukumbu: Sumaye Kujitoa Chadema

Jana, Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye alitangaza kujiondoa Chadema, chama alichojiunga nacho mwaka 2015.

Mie mtumishi wako nilibashiri tukio hilo hivi majuzi tu, Novemba 30

Mengine nayoweza kubashiri bila shaka ni pamoja na

(a) Licha ya Sumaye kudai kuwa hatojiunga na chama chochote, atatangaza kujiunga na CCM kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Vilevile yeye na Lowassa watatumiwa na CCM “kuwaeleza Watanzania kuhusu maovu ya Chadema” kabla na wakati wa kampeni.

(b) Kuna angalau wabunge wawili wa Chadema watakaotangaza kujiunga na CCM hivi karibuni.

Naandika haya nikiwa nimekunja uso kwani si habari njema. Upinzani imara ni muhimu mno kwa ustawi na mustakabali wa Tanzania yetu.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali