"Kutekwa" Soka na wenzake: Huenda vijana wao wakatukana, lakini ukweli ni kwamba Chadema wanarudia kosa walilofanya baada ya Ben Saanane "kupotea"
Hiki ni kipindi kigumu sana kwa watu kama Jasusi ambao hawajihusishi na vyama vya siasa. Ni kipindi kigumu kwa sababu, mtu asiye na chama akilogwa kufanya jambo linaloonekana kuwa na manufaa kwa CCM, ategemee mvua ya matusi kutoka kwa wafuasi wa Chadema.
Na akiona kuna umuhimu wa kufanya jambo lenye maslahi kwa upinzani hususan Chadema, wafuasi wa CCM n…