Kung'olewa kwa Sheikh wa Mkoa wa Dar Alad Musa: mwisho au mwanzo wa mtafaruku BAKWATA?
Nini? Jana Februari 2, ilitolewa taarifa kwamba Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) katika kikao chake kilichofanyika siku mbili chini ya Mwenyekiti wake, Mufti Abubakar Zubeir limetengua uteuzi wa Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum kuanzia (jana) Februari 2, 2023.
Kwanini? Taarifa husika haikueleza sababu za ha…