Kumbe Katibu Mkuu mpya Mambo Ya Ndani ni mshkaji wa Jiwe kitambo

Kuzungukwa na washkaji na "mapoti zake" kwaweza kuchangia anguko lake

Naomba ieleweke kuwa hakuna sheria inayomkataza Rais kuteua marafiki zake. Na pia hakuna sheria inayotamka bayana kwamba teuzi za Rais zisielemee mkoa/kanda/kabila flani tu.

However, busara kidogo tu zingetosha kumfahamisha Rais Magufuli kwamba japo sheria haikatazi kujaza marafiki au watu kutoka mkoa/kanda/kabila flani tu, kuna athari kadhaa kufanya hivyo.

Moja ilimkuba Magufuli mapema tu. Mmoja wa maswahiba wake wakubwa, Kitwanga, alimpuuza bosi wake (Magufuli) hadi akawa analewa wakati wa kazi. Waziri mwenye kuongoza moja ya wizara nyeti kwa usalama wa raia na nchi, anaingia bungeni akiwa bwii.

Baadhi yetu tulimpongeza alipomtimua Kitwanga, kwa sababu yahitaji ujasiri kumtosa swahiba, lakini pia pongezi hizo ziliambatana na matumaini kwamba Magufuli angeepuka kuendekeza “ushkaji.”

Lakini tangu wakati huo hadi muda huu, Magufuli ameendelea kutumia kigezo cha ushkaji, ukabila, ukanda na hata udini kwenye teuzi zake mbalimbali.

Mmoja wa majaji ni mkwewe ilhali Katibu Mkuu Hazina (mlipa pesa mkuu wa serikali) ni mpwae.

Ukihesabu idadi ya mawaziri na manaibu, makatibu wakuu na manaibu, wakurugenzi wa wizara, wakuu wa mikoa na wilaya, RAS na DAS, na viongozi mbalimbali wa umma wanaoteuliwa na Rais, asilimia kubwa ni watu wa kabila moja nae, na hivyo wanatoka nae kanda ya Ziwa aka “Kanda Maalumu,” na idadi ya Waislamu ni haiwiani na wasio Waislamu. Nisiume maneno: Magufuli ni mkabila, anaendekeza ukanda na “ushkaji,” na mdini pia.

Enewei, lengo la makala hii ni hilo kwenye kichwa cha habari. Nimefahamu kuhusu habari hiyo baada ya kuiona huko Jamii Forums

Good news is, anguko lake linaweza kuchangiwa na kuzungukwa na washkaji, “piti zake,” na watu kama akina Bashite ambao wapo kimaslahi zaidi na kamwe hawawezi kumwambia Magufuli kuwa “mzee hapa kuna walakini.”

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali