Kuibuka kwa Dkt Mpango: tatizo sio serikali kutotolea maelezo alikuwa wapi, tatizo ni kusherehesha uzushi, matusi na tabia mbaya mtandaoni
Aliyemzushia kifo Dkt Mpango alishafanya hivyo tena Oktoba 2020 lakini si jamii wala serikali iliyomkemea.
Hatimaye Makamu wa Rais Dokta Philip Mpango alijitokeza hadharani jana ambapo awali alihudhuria misa ya Jumapili huko Dodoma kabla ya kwenda Ikulu ya Chamwino ambako alikutana na Rais Samia Suluhu na kuongea kidogo.
Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa Dokta Mpango kuzushiwa kifo. Na mara zote, chanzo cha uzushi huo ni mtu yuleyule.
Lakini kabla ya k…