Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: Vitu 15 vya Kufanya "Kutuliza Akili."
Udogoni niliishi jirani na mtu mmoja ambaye kwa viwango vya kijijini alikuwa tajiri mkubwa. Na kutokana na utajiri wake, hata akijibu shikamoo, ilikuwa big deal.
Fast forward miaka kadhaa baadaye, niliporudi kijijini kwa likizo kutoka Ughaibuni, tajiri yule alinialika kupata mlo nae nyumbani kwake. Ilinitafakarisha sana kuhusu jinsi mabadiliko kwenye “social status” yanavyofanya kazi hususan vijijini.
Long story short, mwaliko huo ulikuwa fursa muhimu kwangu kumdadisi swali ambalo nilikuwa najiuliza muda mrefu: how is it like kuwa tajiri. Yaani like tajiri anaamkaje asubuhi? Ana hofu kama masikini asiyejua mlo wake utakuwaje? Analala kama maskini asiyejua kesho yake itakuwaje?
Alichonieleza kimebaki kichwani hadi leo. Aliniambia kuwa ni kweli utajiri una raha zake, tena nyingi tu, lakini wasichofahamu watu wengi ni kwamba utajiri pia una changamoto nyingi tu.
Akanipa mfano halisi. Yeye alikuwa na malori yanayosafirisha mizigo sehemu mbalimbali. Akanieleza kuwa moja ya vitu vinavyomnyima usingizi ni hofu ya kuamka na kuambiwa “bosi lori limetekwa na majambazi” au “lori limepata ajali.” Akasema muda pekee anaolala kwa amani ni pindi malori yake yote yakirudi salama.
Lakini napo pia anakuwa na hofu nyingine ya lini atapata tenda ya kusafirisha mizigo mingine. Akatanabaisha kuwa kuwa hofu hiyo ni sehemu tu ya “utumwa wa pesa” unaowakabili matajiri ambapo takriban muda wote wanafikiria kuhusu pesa. Aidha kuziongeza au hofu ya kuzipoteza.
Lengo la somo hili sio kuongelea utajiri bali kukumbushia kuwa kama wanadamu wengine, hawa wenzetu wanaojimudu kimaisha hukumbana na changamoto zinazoweza kufanya “akili ichoke.”
Kwahiyo, bila kujali unajimudu kimaisha au unasuasua, vitu hivi 15 (vipo vingi zaidi ya 15) vitakusaidia kutuliza akili
Sikiliza muziki tulivu. Kama hakuna muziki, sikiliza “sauti za asili” kama vile sauti za ndege, bahari, nk.
Pata kinywaji. Simaanishi pombe bali maji baridi, juisi ya asili, nk
Pumzika. Na usipumzikie kwenye mitandao ya kijamii. Itakuumiza kichwa kuliko hicho kinacholazimisha utulize kichwa
Vuta pumzi ndefu, toa pumzi ndefu. Kwa sekunde chache tu.
Andika kitu chochote kile. Pengine hicho kinachoumiza akili yako.
Jaribu kutengeneza mpango wa kukabili changamoto husika. Je linalokutatiza ni la lazima sana kiasi haliwezi kuahirishwa au kuachwa kabisa? Hakuna njia mbadala?
Fanya tahajudi
Angalia video za kuchekesha
Nusa maua yenye harufu nzuri kaka vile waridi
Nawa uso na maji baridi au ya vuguvugu.
Tembea kidogo japo dakika chache
Tafakari kuhusu ulivyonavyo na ambavyo wengine hawana badala ya kuangalia tu usivyonavyo
Tafakari: je wewe wa leo ni bora au ovyo zaidi wa wewe wa jana, wiki iliyopita, mwezi uliopita, mwaka uliopita, miaka kadhaa iliyopita, nk?
Tenda wema. Kwa mfano nenda hospitali kutembelea wagonjwa hata usiowajua. Au tembelea yatima.
Sali.
Nakutakia wikiendi njema