Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: tenga wasaa wa kujipongeza
Mie kocha wako ni mmoja wa Watanzania wanaoongoza kwa kutukanwa mtandaoni. Baadhi ya wanaonitukana nawafahamu japo idadi kubwa ni watu nisiowajua. Kosa langu pekee linalosababisha nitukanwe mara kwa mara ni kutumia haki yangu ya kikatiba na wajibu wangu wa kiraia kusema kile nachoamini ni kweli.
Well, pengine nachoona ni kweli ni uongo kwa mtu mwingine. Hata hivyo, kwa vile huafikiani nami haimaanishi nastahili kutukanwa.
Watanzania wengi wanapenda matusi kama wanavyopenda ubuyu. Na njia rahisi ya kuwa maarufu katika Tanzania ni kutukana sana kama Kigogo au mrithi wake Martin, au kuwapa watu dozi kubwa ya ubuyu kila siku.
Jana nilikuwa naangalia twiti moja ya mtu aliyenitukana. Ilikuwa na likes zaidi ya 600. Kichekesho ni kwamba zaidi ya nusu ya likes hizo ni watu wanaonifolo.
Sasa kila napokutana na matusi dhidi yangu huwa kwa sekunde kadhaa najiskia vibaya kama mwanadamu mwingine. Kwa sekunde hizo huwa najikuta nasahau mazuri mengi nayoyafanya kwa ajili ya umma ikiwa ni pamoja na hizi kozi za bure.
Lakini mara zote, baada ya sekunde hizo chache za masikitiko/maumivu, huwa natafuta kitu japo kimoja chanya cha kunifanya nijiskie fahari. Na kwa bahati nzuri nina lundo la vitu navyoweza kujivunia navyo.
Na kwa vile Watanzania wengi ni wachoyo wa pongezi isipokuwa kwenye mambo wanayoyapenda kama vile ubuyu na matusi, ukisema usubiri kupongezwa kwa hili au lile, utazeeka huku unasubiri pongezi hizo.
Muda mwingi tunautumia kujilaumu au kulaumu wengine. Lakini hata kwa wale wasio wachoyo wa pongezi, ni nadra kwao kujipongeza.
Basi kuanzia leo, anza kutenga muda japo mara moja kwa wiki kama sio mara moja kwa siku kujipongeza kwa hili au lile. Waweza kujipongeza kwa kuwa muungwana, kwa kukemea maovu, kwa kuwa karibu na Mola wako, kwa kuwasaidia wenzetu wenyw uhitaji, kwa kufundisha au kuhabarisha au hata kuburudisha, kwa kufanya jambo linalokuomgezea u-mtu bora wako, na kadhalika na kadhalika.
La muhimu uanze leo. Na kumbuka kuwa haba na haba hujaza kibaba. Kwa kimombo wanaita “baby steps” yaani “mdogomdogo” kwa lugha ya mtaani. Yes, hatua moja kila siku ni hatua saba kwa wiki. Jambo dogo leo, na dogo kesho, na keshokutwa, nk muda si mrefu utakuwa umepiga hatua kubwa.
Siku njema
Create your profile
Only paid subscribers can comment on this post
Check your email
For your security, we need to re-authenticate you.
Click the link we sent to , or click here to sign in.