Barua Ya Chahali

Share this post
Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: jifunze kupuuza watu wanaopora amani yako/vitu vinavyoiba furaha yako
www.baruayachahali.com
AdelPhil Online Academy

Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: jifunze kupuuza watu wanaopora amani yako/vitu vinavyoiba furaha yako

Evarist Chahali
Apr 20
Share this post
Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: jifunze kupuuza watu wanaopora amani yako/vitu vinavyoiba furaha yako
www.baruayachahali.com

Kitambo sijaweka somo kwenye kozi hii endelevu. Ni kutokana na kutingwa na majukumu mengine.

Kama unamfuatilia kocha wako kwa muda mrefu, utakumbuka kuwa alishaeleza kuwa anapenda kutumia mifano inayomhusu yeye mwenyewe.

Na somo la leo linatumia njia hiyo.

Kuna msemo ambao kocha wako amekuwa akiutumia mara kwa mara hususan kwenye mtandao wa kijamii wa Twita

Twitter avatar for @Chahali𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 @Chahali
Ukitaka kumuua mbu, mnyime access to damu. Likewise, ukitaka kumdhibti attention seeker, mnyime attention.
Image

December 19th 2017

5 Retweets24 Likes

Kocha wako ni mtu anayeandamwa sana na wakorofi mtandaoni. Sasa kufahamu tatizo ni suala moja, na kujua jinsi ya kukabiliana nalo ni suala jingine kabisa. Hata hivyo, kama ilivyotajwa mara kadhaa, kutambua tatizo ni hatua muhimu katika kuelekea kulitatua.

Moja ya mbinu muhimu anayotumia kocha wako ni kuwapuuza wakorofi hao. Kwa sababu kiukweli, sababu kubwa ya watu kufanya usumbufu mtandaoni ni kutaka attention. Hali ni mbaya zaidi kwa watu wenye followers wengin, kwani baadhi ya wakorofi wanafahamu bayana kuwa ukiwajibu, unakuwa kama umempiga chura teke. Wanapata umaarufu wasiostahili.

Kuna njia mbalimbali za kuwapuuza. Moja ni hiyo ya kujifanya kama hujaona kilichoandikwa. Lakini tatizo la njia hii ni kwamba wahusika wanaweza kuhamasika kuendelea kukusumbua “mpaka uone.”

Kama usumbufu si mkubwa sana, njia ya pili ni kutumia kitufe cha kuwanyamazisha, kwa kimombo “mute button.” Watapiga kelele mpaka wataishiwa sauti ilhali huoni wanachosema.

Ya tatu, na mwafaka zaidi ni kuwapa bloku. Ni mwafaka zaidi kwa sababu kadhaa, lakini mbili za msingi ni hizi. Kwanza, bloku inamnyima mkorofi fursa ya kuona unachoandika. Na kama unaandika vitu vya msingi, mkorofi ananyimwa access ya vitu hivyo, unless atumie akaunti feki, which again ni kama anajiadhibu.

Pili, bloku inauma. Ndio baadhi ya watu waliopigwa bloku na kocha wako miaka kadhaa iliyopita, bado wanalalamika hadi leo, huku baadhi yao wakimtuhumu kocha wako kuwa “anabloku kila mtu.”

Barua Ya Chahali
Shutuma kuwa "nimebloku kila mtu" si za kweli: maelezo ya jinsi navyotumia kubloku kama "kinga yangu" dhidi ya watukanaji na "watu wanaohusiana na kitengo."
Jana nilipewa heshima na blogu ya DarMpya ambapo waliniomba kuwa “host” kwenye mjadala wa TwitterSpaces kuhusu binti wa Kinaijeria aitwaye Zainab, ambaye anadai kuwa alinisurika kubakwa alipokuwa mapumzikoni Zanzibar…
Read more
23 days ago · 3 likes · Evarist Chahali

Kama hujawahi kusumbuliwa mtandaoni, huwezi kuelewa umuhimu wa kubloku wakorofi.

Lakini bila shaka unaelewa umuhimu wa “kubloku watu katika maisha yetu halisi mtaani.” Ni mara ngapi unakwepa mtaa flani kwa sababu kuna genge la vijana ambalo kila likikuona linataka kukusumbua?

Ni mara ngapi unamkwepa mtu ambaye kila anapokutana nawe anataka aidha kushusha utu wako au kukufanya ujisikie vibaya?

Ni mara ngapi unabadili chaneli ya runinga yako kwa sababu kuna mtangazaji anakukera?

Hatua hizo hazina tofauti na kupuuza wakorofi mtandaoni. Na by kupuuza, namaanisha hatua hizo tatu nilizozitaja hapo juu - jifanye kama hujaona, zuwia kuona kwa kutumia kitufe cha kunyamazisha (mute button) na kama ni usumbufu mkubwa, mlime mtu bloku.

Sio kama kocha wako anakuambukiza tabia mbaya, anakufunza jinsi ya kulinda amani ya nafsi/akili yangu, Waingereza wanaita “peace of mind.” Kamwe usiruhusu mtu yeyote kupora amani/ furaha yako.

Lakini pia somo la leo linaweza kuwa muhimu kwa hao wanaolalamika kuhusu kupigwa bloku. Hivi ni mara ngapi unatamani kufahamiana na mtu flani maarufu lakini anajifanya kama hakuoni? Au ni mara ngapi umesimama mstari wa mbele kumuunga mkono na kumshabikia kiongozi wa kisiasa lakini hajawahi kukutambua hata mara moja?

Ofkoz, mara nyingi watu hukimbilia kuwatetea “watenda dharau hao” kuwa “ah yule ana mashabiki/wafuasi wengi, sio rahisi kuniona.” Au “yule ni mtu muhimu sana, yupo bize, ndio maana hajanitambua.” Ukweli mchungu ni kwamba amekudharau tu.

Kocha wako anayetuhumiwa “kubloku kila mtu” ana followers zaidi ya 192,000 huko Twitter na takriban 50,000 huko instagram. Lakini kila siku ya Mungu hujibidiisha kujibu, ku-like au kuritwiti kila bandiko linalomtaja. Na huona kama ametenda dhambi kubwa kutofanya hivyo. Kadhalika, licha ya kupokea DMs lukuki takriban kila siku ya Mungu, hujibidiisha kuwajibu wahusika mapema kadri iwezekanavyo.

On equal measures, hukuchukua hatua stahili dhidi ya kila mkorofi anayejaribu “kuchafua hewa.”

Kocha wako anahitimisha somo hili kwa kukupatia moja ya machapisho bora kabisa kuhusu “jinsi ya kuishi kwenye dunia iliyojaa wakorofi na wasumbufu.” Chapisho hili, 48 Laws of Power, linajikita kwenye ukweli kwamba tofauti na busara za wahenga kuwa dunia imejaa watu wema, ukweli ni kwamba kuna maharamia wengi tu ambao ukiwapa fursa, watakuumiza.

Siku nyingine kocha wako atakupa link ya kupakua kitabu kingine bora kabisa cha kukuwezesha kumudu maisha katika dunia yenye changamoto lukuki. Kinaitwa “The Subtle Art of Not Giving a F*ck.”

Na wakati mwingine, kocha wako atakupatia link ya kupakua kitabu hiki cha mwandishi huyohuyo Mark Manson

Na kukuimarisha, kuna chapisho jingine bora kabisa la STOICISM

Mwisho, kwa wageni kwenye kozi hii, anayeitwa “kocha” ni mie mtumishi/jasusi wako. Kwanini “kocha”? Kwa sababu katika kufundisha kozi hii ya Jinsi ya Kuwa Mtu Bora, ninajivika “ukocha wa maisha” kwa kimombo wanaita “life coach.”

Siku njema

Share
Share this post
Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: jifunze kupuuza watu wanaopora amani yako/vitu vinavyoiba furaha yako
www.baruayachahali.com
TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing