Barua Ya Chahali

Share this post
Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: Jifunze "baraka za kufeli" kutoka kwa galacha wa Formula One Lewis Hamilton
www.baruayachahali.com
AdelPhil Online Academy

Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: Jifunze "baraka za kufeli" kutoka kwa galacha wa Formula One Lewis Hamilton

Evarist Chahali
Mar 15
Share this post
Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: Jifunze "baraka za kufeli" kutoka kwa galacha wa Formula One Lewis Hamilton
www.baruayachahali.com

Maisha yangekuwa mazuri sana laiti tungefaulu kwenye kila jambo. Lakini maisha hayapo hivyo. Takriban kila mwanadamu ameshawahi kufeli, anafeli muda huu au atafeli huko mbeleni. Tofauti tu ni kwenye jinsi ya kufeli, athari za kufeli huko, namna ya kujinasua, nk.

Lakini pia uzito wa kufeli hutegemea pia umaarufu wa mtu japo kimsingi mikakati ya kukabiliana na kufeli haijali wewe ni maarufu au la. Huenda umesahwahi kusikia jina LEWIS HAMILTON. Huyo ni mwanamichezo maarufu kabisa duniani kwenye mashindano ya magari ya Formula One.

Katika msimu uliopita, Hamilton ambaye mara kwa mara amekuwa akikumbana na ubaguzi wa rangi hasa kwa vile mchezo huo wa mashindano ya magari ni wa “wazungu weupe,” alikuwa katika nafasi ya kuweka historia nyingine ya kutwaa nafasi ya kwanza, lakini alihujumumiwa waziwazi na mpinzani wake Max Verstappen akatawazwa mshindi katika mchuano wa mwisho huko Abu Dhabi.

Sasa Hamilton anakiri kwamba “kushinda sio kila kitu” (winning isn’t everything). “Wakati mwingine unafeli, na unakua bora zaidi na huo ni ushindi pia,” anasema mwanamichezo huyo Muingereza.

“Ushauri wangu kwa watu ni kwamba kamwe usiogope kufeli, kwa sababu ni lazima utafeli ukiwa njiani kuelekea kwenye mafanikio.”

Kocha wako huwa napenda kukumbushia kuwa njia mwafaka zaidi ya kudili na kufeli ni kwa kuchukulia kufeli huko kama kuni za kuchochea moto wako wa kufikia lengo kusudiwa.

Siku njema

Comment
Share
Share this post
Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: Jifunze "baraka za kufeli" kutoka kwa galacha wa Formula One Lewis Hamilton
www.baruayachahali.com

Create your profile

0 subscriptions will be displayed on your profile (edit)

Skip for now

Only paid subscribers can comment on this post

Already a paid subscriber? Sign in

Check your email

For your security, we need to re-authenticate you.

Click the link we sent to , or click here to sign in.

TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing