Kozi ya #JinsiYaKuwaMtuBora: "Attention Economy" - Tunaishi Zama Ambazo "Attention" Ina Thamani Kama Pesa. Njia Mbili Muhimu Za Ku-"Control Attention."
Kuna kitu kinaitwa “attention economy” ambacho kina umuhimu mkubwa katika zama hizi za mapinduzi ya teknolojia.
Kwa kifupi, kitu hiki kinamaanisha kuwa “attention” - ile hali ya kutumia muda wako kwa mtu au kitu flani - ni kama bidhaa ghali.
Kuelewa maana yake, angalia watu wanaoitwa “social media influencers.” Kutegemea umaarufu na idadi ya followers, baadhi ya watu hawa wanatengeneza mamilioni kwa kutangaza tu bidhaa au huduma mbalimbali.
Makampuni yanahitaji msaada wa influencers hawa kwa sababu wanapewa attention na watu wengi. Kwahiyo kwa kuwalipa, wauza bidhaa/watoa huduma husika wananunua attention ya followers wa influencer husika.
Hata hicho kinachoitwa “uchawa” hakipo mbali na wanayofanya hawa influencers. Chawa maarufu wamekuwa nyenzo muhimu kwa wasanii wetu kufikisha ujumbe kwa watu mbalimbali. Na takriban chawa wote maarufu wamelamba dili za matangazo ya taasisi mbalimbali. Utasikia sijui balozi wa hiki, au kile. Ni kwamba chawa anatumika kuvuta attention yako.
Lakini hata bila kuwa na thamani ya pesa, attention ni muhimu kwa mtu binafsi hususan katika “jinsi ya kuwa mtu bora.” Kwa mfano, endapo unakabiliwa na mtihani, halafu attention yako ipo kwenye ubuyu insta, unajua matokeo yake yatakuwaje.
Kadhalika, kutoa attention yako kwa mtu asiyestahili itaishia tu kukuumiza akili.
Kuna unyanyasaji mtandaoni ambapo kna watu wanaitwa TROLLS, kama alivyokuwa Mlawa aka Kigogo kabla hajatalikiana na Chadema. Hawa trolls wanahangaika sana na attention yako. Wanasema hili, wanazusha lile, ili mradi tu uwape attention, na waweze kukuumiza. Ndio maana moja ya nyenzo muhimu dhidi ya wasumbufu wa mtandaoni ni kuwapiga bloku.
Twende kwenye njia mbili muhimu za ku- “control attention.” Lakini kabla ya kuziongelea, nitanabaishe kuwa tunaishi zama ambazo ni rahisi mno kushindwa kumiliki attention yako. Unaingia mtandaoni unakutana na vichwa vya habari vya kuvutia kama sio vya kutisha, unabonyeza link au kuangalia video husika, na kama si mwerevu huwezi kubaini kuwa umeingizwa mkenge.
Ukienda YouTube utakuna na lundo ka video zenye habari feki, kwa mfano “Magufuli aliuawa kwa kunyweshwa sumu” na uzushi kama huo. Kuweka kichwa cha habari cha kizushi kwa minajili ya kupata likes au views hufahamika kama “clickbait” kwa kimombo.
Njia mbili za kukusaidia ku-control attention.
Control factors zilizo nje yako (external factors): Hapa kuna vitu viwili.
Kwanza ni teknolojia. Hili halihitaji maelezo. Runinga “kukuibia” attention yako, ubuyu insta, video mbalimbali YouTube au Facebook, nk.
Pili ni mazingira: Hapa ni vitu kama watu ambao kwa namna moja au nyingine wanachukua attention yako. Haimaanishi kuwa ni kitu hasi kumpa mtu attention bali je kufanya hivyo kuna tija yoyote kwako?
Control factors zilizo ndani yako (internal factors):
Hapa kuna vitu viwili. Cha kwanza ni tabia yako. Unapoamka asubuhi, attention yako ipo kwenye nini? Muda huu unasoma kozi hii, nini kinakushawishi uachane nayo ili uwekeze attention yako huko?
Cha pili ni fikra zako. Kwa kiasi kikubwa furaha na majonzi yetu huchangiwa na fikra zetu. Unaweza kuwa na majonzi kwa kitu ambacho hakikuhusu kabisa. Au unaweza kuwa na furaha kwa jambo lisilohusiana nawe.
Unaweza kuwa na hofu kuhusu kesho, lakini kama mwanadamu yoyote yule, huna uwezo wa asilimia 100 ku-control yatakayojiri kesho. Sanasana unaweza tu kujiandaa. Lakini hata ukijiandaa vipi, yawezekana kweli kujipanga dhidi ya ajali, kwa mfano?
Natumaini somo hili litakuwa na msaada kwako.
Uwe na Jumapili njema