Kozi ya BURE ya Open Source Intelligence #OSINT: "kuficha ushahidi" na kutengeneza utambulisho feki (Sock Puppets)
Kwanza samahani kwa kuchelewa kuwaletea somo hili ambalo lilipaswa kuwa hewani Jumanne lakini ikashindikana kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa mkufunzi.
Pili, kama ilivyoelezwa awali, mtaala wa awali unaweza kubadilika kwa sababu moja au nyingine, kubwa zaidi ikiwa kuhakikisha kuwa masomo yanaeleweka badala ya kumchanganya “mwanafunzi.”
Ni kwa mantiki hiyo, somo la sita litahusu katika maandalizi ya uchunguzi wa OSINT. Somo la saba litahusu kitu kinachoitwa “sock puppet” yaani kwa tafsiri isiyo rasmi, “utambulisho feki” ambao utalazimika kuutumia unapofanya uchunguzi wako wa OSINT.