Knowledge is Power: Jinsi Ya Kutafuta/Kupata/Kuhakiki Taarifa kuhusu #Coronavirus

Baada ya mada ya utambulisho, twende kwenye mada nyingine katika mwendelezo (series) huu wa mada za "kukujengea uimara katika nyakati za hofu/shaka kama zama hizi za janga la korona."

Lakini kabla sijaingia kwenye mada naomba kukusisitiza kitu kimoja muhimu. Afya yako si ya Magufuli wala serikali yake. Usiruhusu wakupangie nini cha kusoma/kutazama/kusikiliza.

Natoa tahadhari hii baada ya kuona post hapa insta ya msanii mmoja maarufu wa kike akieleza "namna serikali yetu inajitahidi kuwakinga wananchi wake dhidi ya korona."

Msifanywe mafala (ashakum si matusi), serikali inayojitahidi kuwakinga wananchi wake dhidi ya korona haiwezi kutumia wasanii waipigie debe.

Naambiwa na watu kadhaa kuwa huko mikoani wamepigwa marufuku kuongelea korona ilhali watumishi wa afya wamezibwa mdomo wasiseme kama kuna wagonjwa kwenye hospitali zao.

Enewei, twende kwenye mada husika. Licha ya serikali na wapambe wake kujikabidhi hakimiliki ya kuzungumzia korona na afya zenu, haimaanishi usifanye jitihada binafsi kufahamu ukweli.

Kumbuka suala hili linahusu afya yako binafsi, sio ya Jiwe au ya wasanii wake. Ni jukumu lako kupata taarifa sahihi ili uweze kujikinga na janga hilo.

Lakini ili uweze kupata taarifa sahihi shurti ujue namna ya kuzipata na wapi pa kuzipata. Lakini pia hata ukijua namna ya kupata/wapi pa kupata taarifa husika, unapaswa pia kuhakiki kama ni sahihi/za kweli au la.

Ni kama kutafuta maana ya neno kwenye kamusi. Kama hujui linavyotamkwa hutopata maana husika.

Kwahiyo basi, jihukumu mwemyewe: jiulize "je najua wapi pa/jinsi ya kupata taarifa sahihi kuhusu korona"?

Jiulize pia "je najua jinsi ya" kutofautisha pumba na mchele" (aani kutofautisha kati ya ukweli na matango pori)?

Kama hujui, basi usisite kuomba msaada. Nasisitiza hili kwa sababu wanasema kwa kimombo "knowledge is power," yaani "uelewa unakupatia nguvu." Na njia ya kujenga uelewa ni elimu, sio lazima ya shule/chuo bali kujielimisha mwenyewe. Usione aibu kuuliza.

Mwisho, mie si mtaalam wa afya. However, najibidiisha kuelewa vitu vingi. Na ukiniuliza kitu nisichoelewa najua wapi pa kukutafuta au nani wa kumuuliza.

Jikinge dhidi ya korona na wakinge na wenzako pia.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali