Kitabu cha kielektroniki (ebook)

Kitabu cha kielektroniki (ebook) kilichoandikwa na mtumishi wako #EvaristChahali kitakuwa tayari Septemba mosi. Kinahusu mbinu mbalimbali za kimaisha za kukuwezesha kuwa mtu bora au kama tayari ni mtu bora, basi mbinu zilizomo katika kitabu hiki zitakusaidia kuboresha ubora wako. Neno la Kiingereza ni “personal development” yaani tija (productivity), hamasa (motivation), mbinu za maisha (lifehacks), kupata/kuboresha ujuzi (skills) na kuibua vipaji (talents), nk

Kitabu cha kielektroniki (ebook) maana yake ni kwamba unaweza kukisoma kwenye simu yako au tablet yako au kompyuta yako... kama unavyosoma post za hapa insta.

Pre-orders zinakaribishwa. Ni sh 5,000/= tu

Pia maoni yanakaribishwa kuhusu hiyo cover/mwonekano

Uwe na siku na wiki njema.

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali