Shutuma kuwa "nimebloku kila mtu" si za kweli: maelezo ya jinsi navyotumia kubloku kama "kinga yangu" dhidi ya watukanaji na "watu wanaohusiana na kitengo."
Jana nilipewa heshima na blogu ya DarMpya ambapo waliniomba kuwa “host” kwenye mjadala wa TwitterSpaces kuhusu binti wa Kinaijeria aitwaye Zainab, ambaye anadai kuwa alinisurika kubakwa alipokuwa mapumzikoni Zanzibar.

Darmpya Blog @darmpya_
Join me in my Space! https://t.co/zRxrn9bBglLakini mara baada ya blogu hiyo kutangaza kuwa watakuwa nami kwenye shughuli hiyo, kulijitokeza lundo la watu waliolalamika, na wengine kutukana kabisa, kuhusu “Chahali anayebloku kila mtu.”
Ni wazi kuwa ningekuwa nimebloku kila mtu, ndugu zangu wa DarMpya wasingeweza kuwasiliana nami kuhusu ku-host hiyo TwitterSpaces.
Lakini kubwa zaidi, hadi wakati naandika makala hii nina followers 192,702 huko Twitter, na kwa wastani kwa siku ninapata followers 100 hivi. Sasa huhitaji kuwa mchunguzi kubaini kuwa “mtu anayebloku kila mtu” hawezi kuwa na idadi hiyo “si haba” ya followers.


Lolo ☘ @PhentyKiria
@Chahali Sijui sasa, nimeuliza tuLengo la makala hii sio kueleza kuhusu idadi ya followers nilionao bali kuzungumzia kwa kifupi tuhuma za “mie kubloku kila mtu.”
Ni kweli kwamba nimebloku watu wengi. Lakini sijawahi kumbloku mtu bila sababu. NEVER.
Kuna makundi mawili ya watu niliowabloku.
Kundi la kwanza ni mahodari wa matusi mtandaoni. Kanuni ya maisha yangu mtandaoni ni rahisi tu: kuwa mstaarabu au kula bloku. Mtu akinitukana, hata awe ni nani, nitampa bloku.
Kwa bahati mbaya - au pengine makusudi - Watanzania wengi wanapenda matusi. Kama sio wao wenyewe kutukana basi kufurahia kuona mtu anatukanwa.
Huko nyuma wakati Didier Abdallah Mlawa aka Kigogo ananitukana kila alipojiskia, maelfu kwa maelfu ya followers wake walikuwa wanashangilia, huku baadhi yao wakimuunga mkono kwa kunitukana pia.
Sasa kuwabloku maharamia hawa ni kosa?
Kundi la pili ni “watu wenye uhusiano na Idara ya Usalama wa Taifa.” Hawa ni asilimia kubwa zaidi ya niliowabloku.
Nikurudishe nyuma kidogo. Nilijiunga Twitter mwaka 2008, mwaka huohuo ambapo uhusiano wangu na kitengo ulivunjika. Kwahiyo wakati najiunga na Twitter, tayari kuna macho yaliyoelekezwa kwenye akaunti yangu kufuatilia natwiti nini. Naamini wengi wenu mlikuwa hata hamuijui Twitter wakati huo.
Pia wakati huo najiunga na Twitter, Tanzania yetu ilikuwa inapitia katika zama ambazo ufisadi ulitawala kila mahala. Hiki ni kipindi cha utwala wa Jk, na kwa hakika hali ilikuwa mbaya sana. Badala ya ku-export mazao, bidhaa iliyoongoza kuwa exported ilikuwa madawa ya kulevya. Na bidhaa iliyoongoza kuwa imported ilikuwa madawa ya kulevya pia. Kwa kifupi, Tanzania ilikuwa moja ya hubs kubwa duniani za biashara hiyo haramu.
Lakini licha ya unga, kulikuwa pia na biashara ya noti feki, biashara ya kusafirisha binadamu (human trafficking), biashara haramu ya silaha, na kila uhalifu ambao unaweza kuufikiria.
Nami nilikuwa miongoni mwa sauti chache kabisa zilizozisikika kukemea ufisadi. Japo kelele hizo zilizoanza rasmi mwanzoni mwa mwaka 2006 zilichangia kugharimu ajira yangu huko kitengoni, lakini pia ninafarijika kutanabaisha pasi shaka kuwa zilikuwa na mchango katika kung’oka kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa, Februari 2008, kufuatia skandali kubwa kabisa ya Richmond.
Baada ya Lowassa kung’oka, kelele zangu ziliendelea dhidi ya ufisadi ulioigubika serikali ya Jk, na mwaka 2013 lilifanyika jaribio la kwanza kutoa uhai wangu lakini nikasalimika. Moja ya vitu vya kusikitisha sana kufuatia tukio hilo ni jitihada zilizofanywa na kitengo kutumia mitandao ya kijamii “kuua” stori hiyo. Yaani baada ya kushindwa kuniua, wakaamua kuua maelezo yangu.
Mwaka 2013 na 2014 ilikuwa kipindi mgumu sana, na almanusra nijiondoe moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii. Kipindi hicho, kulikuwa na genge la vijana ambao walijipa hakimiliki ya “Twitter ya Tanzania” ambapo walitisha watu, walitukana watu, walidhihaki watu, na unyanyasaji huo wa mtandaoni ulifikia kiwango cha juu zaidi hadi mmoja ya wana-Twitter maarufu wakati huo, Betty Ndejembi, alipoamua kujiua mwaka 2014 kutokana na bullying.
Kwa hakika mwaka 2014 ulikuwa mgumu sana katika historia ya “Twitter ya Tanzania.”
Nami niliendelea kuwa mmoja wa wahanga wakubwa wa unyanyasaji wa mtandaoni. Yaani kuna wakati nilikuwa naingia Twitter kwa kuchungulia, maana matusi, kashfa, uzushi, na kila baya dhidi yangu ilikuwa ni mara kadhaa kila siku.
Kwa bahati nzuri, katikati ya 2014 mwanasiasa kijana , January Makamba akatangaza nia ya kuwania urais.
Kabla ya January kutangaza nia ya urais, neno “mwanaharakati” lilikuwa kama tusi, na wanyanyasaji hao wa mtandaoni walilitumia kutuandama sie “wapiga kelele.”
January aliwavuta vijana wengi kuingia kwenye siasa, na taratibu neno “mwanaharakati” likaanza kuwa na taswira chanya kidogo. Kadhalika, wengi wa vijana waliovutiwa na masuala ya siasa baada ya January kutangaza nia, walikuwa kwenye genge la wanyayasaji wa mtandaoni.
Sijui bila January kuwavutia vijana hao kuingia kwenye siasa hali ingekuwaje.
Mwaka mmoja baadaye, 2015, kulikuwa na matukio mengi japo unyanyasaji wa mtandaoni ulikuwa nafuu sana. Katikati ya mwaka huo, Lowassa alijiondoa CCM na kujiunga na Chadema. Mie ambaye muda huo nilikuwa naiunga mkono Chadema kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi, nililazimika kuvunja urafiki na chama hicho kwa sababu ya Lowassa.
Na baadaye nilifuatwa na baadhi ya viongozi wa CCM kunisihi nitoe huduma ya usadi wa kisiasa (political consulting) kwenye mitandao ya kijamii kwa kigezo kwamba “sote - mie na CCM - adui yetu ni mmoja, yaani Lowassa.” Nikashiriki kampeni ya kumnadi Magufuli.
Kitendo cha kumuunga mkono Magufuli kilipelekea mie kuwa mmoja wa walengwa wa matusi mfululizo kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema. Moja ya matukio yaliyonisikitisha sana ni baada ya kifo cha baba yangu Julai 2015, January alinipa rambirambi ya sh 500,000 na familia ikaomba nimshukuru hadharani. Yeriko Nyerere akakebehi wema huo wa January na kudai “nimeuza uhai wa baba yangu kwa CCM.” Huyu nae ukimbloku bado kuna watu watalaumu.
Nilimnadi Magufuli huku nikimwagiwa mvua ya matusi na wana-Chadema lakini ndio siasa zetu hizo.



Magufuli “alipobadilika” mwishoni mwa mwaka 2016, nikalazimika kurudi kwenye harakati za kukemea maovu yaliyokuwa yanafanywa na utawala wake. Na hii ikanirudisha tena kwenye zama za kunyanyaswa mtandaoni, ambapo safari hii kulikuwa na kikosi maalum cha Idara ya Usalama wa Taifa dhidi ya “wakorofi” kama mie. Kikosi hiki ndio MATAGA.
Na kukajitokeza haramia mkubwa kabisa aitwaye Musiba ambaye alitumia magazeti yake na chaneli yake ya YouTube kunichafua takriban kila wiki. Na kwa vile Waingereza wanasema “misfortunes come in series” (majanga huongozana), dada mmoja wa hapa Uskochi aliyekuwa rafiki mwema, akaungana na watesi wangu na kuanzisha kampeni ya matusi tangu Disemba 2018 hadi hivi leo. Alizusha kila baya aliloweza kunizushia hadi kunizushia kifo cha korona.
Kwa kifupi haya ndo maisha yangu mtandaoni. Kama Mtanzania pekee anayefahamika kuwa mtumishi wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa, huku Idara hiyo ikihangaika kuniondoa duniani, nalazimika kuchukua kila hatua iwezekanayo kuhakikisha usalama wangu.
Na kwa vile maisha yetu mtandaoni yanashabihiana na maisha yetu mtaani, usalama wangu mtandaoni ni muhimu kama usalama wangu mtaani.
Na moja ya nyenzo zinazonifanya kuwa salama mtandaoni ni kuwabaini watu wenye mahusiano na Idara ya Usalama wa Taifa. Siwezi kubainisha nawatambuaje, lakini hao ndio asilimia kubwa ya watu ninaowabloku mtandaoni.
Ili mtu akudukue mtandaoni shurti “akuelewe.” Na njia moja inayotumika kuwaelewa watu mitandaoni ni kuwafolo. Sasa mie nikibaini kuwa “mtu wa kitengo kanifolo” nampa bloku hapohapo.


Kadhalika, ninatumia “apps” za kuhakikisha usalama wa akaunti zangu mitandaoni. Of course, kuna nyakati zinaweza kukosea na kumbloku mtu asiye na hatia lakini ni nadra.
Lengo la makala hii sio kujitetea kuhusu jitihada zangu za kuwabloku wenye matusi na hao watu wa kitengo lakini nimeona si vibaya kuliweka suala hili katika muktadha stahili.