Kila anayeipenda Simba kwa dhati sio tu anapaswa kumsapoti Mo (@moodewji) bali pia kumtetea kwa nguvu zote dhidi ya wazushi wenye ajenda zao binafsi
Inauma. Inakera. Na inasikitisha kuona mtu ambaye sio tu amejitolea fedha nyingi, nguvu nyingi na muda mwingi kuifikisha klabu ya Simba ilipofika leo, namaanisha Mohammed Dewji aka Mo, akiandamwa na watu ambao hawajawahi kuwa na mchango wowote kwa klabu hiyo.
Kuna makundi mawili hivi yanayoendesha kampeni dhidi ya Mo. La kwanza ni watu wanaotamani kuona …