Share this postKamilisha Wikiendi Yako na #UziwaTwita Huu Kuhusu #UshindiMdogoMdogo www.baruayachahali.comCopy linkTwitterFacebookEmailKamilisha Wikiendi Yako na #UziwaTwita Huu Kuhusu #UshindiMdogoMdogo Evarist ChahaliJun 21, 2020Share this postKamilisha Wikiendi Yako na #UziwaTwita Huu Kuhusu #UshindiMdogoMdogo www.baruayachahali.comCopy linkTwitterFacebookEmailEvarist Chahali @Chahali#UziwaTwita mfupi wa kuhitimisha wikiendi yako. Uzi huu unahusu "kusherehekea ushindi mdogo mdogo" kwa kimombo wanasema "celebrating small wins." Evarist Chahali @ChahaliKabla ya kuingia kwenye uzi, nitumie fursa hii katika #FathersDay hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia baba bora kabisa, marehemu Mzee Chahali. Alinifundisha mengi lakini matatu makubwa ni π Kumcha Mungu π Utu na upendo π Kujenga na kustawisha AKILI. Rest in peace, dad!Evarist Chahali @ChahaliTwende kwenye mada. Mara kadhaa nimeongelea umuhimu wa kusherehekea #UshindiMdogoMdogo. Pamoja na faida nyinginezo nyingi, kufanya hivyo husaidia kuleta "ushindi mkubwa." Evarist Chahali @ChahaliYaani "ushindi mdogomdogo + ushindi mdogomdogo + ushindi mdogomdogo + ushindi mdogo mdogomdogo, nk, nk = hatimaye USHINDI MKUBWA. This is no rocket science πEvarist Chahali @ChahaliMara kadhaa nimekuwa nikiweka hadharani matukio mbalimbali ya ushindi mdogomdogo. Lakini bila haja ya kuyarudia matukio hayo, nielekee kwenye ushindi mdogomdogo mpya niliopata wikiendi hiiEvarist Chahali @ChahaliNikurudishe nyuma kidogo. Licha ya mahaba yangu makubwa kwenye masuala ya kompyuta, eneo moja ambalo sikuwahi kuligusa ni kuprogramu kumpyuta (computer programming), yaani kwa kifupi "kuilisha kompyuta maelekezo ya kutekeleza jukumu flani." Evarist Chahali @ChahaliKitu pekee kinachokaribiana na programming ni wakati najifunza kublogu, nililazimika kuelewa "lugja ya kompyuta katika utengenezaji wa blogu," yaani HTML. Japo "wataalamu" wanasema hii sio lugha ya kuprogramu lakini kwangu ilikuwa ni kitu kinachokaribiana na hicho Evarist Chahali @ChahaliBaada ya kuingia kwa kina kwenye #UsalamaWaMtandaoni, moja ya mahitaji muhimu yamekuwa ni msisitizo kwenye kuzimidu lugha za kuprogramu (programming languages), hususan PYTHON. Na niwe mkweli, jina hilo lenye maana ya CHATU kwa Kiswahili liliniogopesha Evarist Chahali @ChahaliLakini kadri nilivyozidi kuzama kwenye #UsalamaWaMtandaoni nikabaini mapema kuwa sio ni muhimu kujifunza Python bali kwa namna flani kama ni lazima. Sasa wikiendi hii nimeanza rasmi zoezi hilo. Si lengo la uzi huu kueleza kwa kina kuhusu kuprogramu au Python bali my small win Evarist Chahali @ChahaliHata hivyo, nimefanikiwa kuelewa masuala kadhaa ya kuvutia kuhusu kuprogramu. Moja ni jinsi ya kujifunza na kuboresha uelewa kuhusu kuprogramu. Njia kuu na pengine rahisi ni kwa kutumia mtandao. Kwa upande wa Python, kuna jamii (community) kubwa iliyo tayari kutoa sapotiEvarist Chahali @ChahaliMwanafunzi wa kuprogramu anakumbushwa kuwa hakuna mtu mmoja mwenye kujua kila kitu kuhusu programming, na hiyo inawafanya hata nguli wa kuprogramu kuendelea kuwa kama wanafunzi. Na hii huondoa dharau kwa wanafunzi halisi pindi wakiuliza "maswali ya kitoto."Evarist Chahali @ChahaliNimejifunza pia njia kadhaa za kuuliza maswali "ki-smati" kuhusiana na kuprogramu. Zipo njia nyingi lakini hizi chache ndio zilizonivutia zaidiEvarist Chahali @Chahaliπ Uliza kuhusu ulichotaka/unachotaka kufanya, na sio tu nini ulichofanya hadi ukakwama. Hii itamsaidia "mwalimu" kujua kama upo njia sahihi au laEvarist Chahali @Chahaliπ Tanabaisha sehemu ambapo ulikutana na kasoro (error) husika. Je ilitokea mwanzoni mwa programu au baada ya kufanya hatua flani?Evarist Chahali @Chahaliπ Copy na paste ujumbe mzima unaoashiria kasoro (error) na "code" yako kwenye tovuti hii pastebin.com au gist.github.com.Discover gistsGitHub Gist: instantly share code, notes, and snippets.gist.github.comEvarist Chahali @ChahaliπEleza nini ulichokwishajaribu kufanya kutatua tatizo husika. Hii huonyesha kuwa wewe si mzembe bali umekwama tu baada ya kujitumaEvarist Chahali @ChahaliπTaja toleo la programu husika. Kuna tofauti katinya toleo la pili la Python na la tatu. Pia tanabaisha OS (Operating System) unayotumia, kama ni Windows au Mac OS au Linux Evarist Chahali @ChahaliπElezea kama kasoro yajitokeza ukifanya hatua flani tu au katika kila hatua unayofanya.Evarist Chahali @ChahaliOfkoz kuna njia zaidi lakini kwa mtazamo wangu, hizi nilizotaja zinafanya zoezi zima la kuuliza na kupewa msaada ulipokwama kiwa rahisi.Evarist Chahali @ChahaliKuna tovuti mbalimbali zinazoeleza jinsi ya kuomba msaada pindi ukikwama kwenye kuprogramu. Hizo ni pamoja na πautbor.com/help/ πreddit.com/r/learnprogramβ¦ π reddit.com/r/cscareerquesβ¦index - cscareerquestionsr/cscareerquestions: A subreddit for those with questions about working in the tech industry or in a computer-science-related job.reddit.comEvarist Chahali @ChahaliWanasema kwamba "programming isn't brain surgery" yaani kuprogramu sio sawa na upasuaji wa ubongo ambao hauna fursa ya kosa japo kiduchu. Kwenye kuprogramu, makosa ni sehemu ya kujifunza.Evarist Chahali @ChahaliNi matarajio yangu kuwa uzi huu utakuhamasisha kuhusu π Ushindi mdogomdogo π Fursa ya kujifunza kuhusu kompyuta hususan #UsalamaWaMtandaoni na pengine kuprogramu pia. Ukihitaji ushauri, usisite kuwasiliana namiEvarist Chahali @ChahaliGood evening Ndimi kocha wako (life coach), Evarist Chahali
Create your profile
Only paid subscribers can comment on this post
Check your email
For your security, we need to re-authenticate you.
Click the link we sent to , or click here to sign in.