Kama huyu kakukera, tafadhali mjulishe

Hii ni email niliyotumiwa na Ndugu Essau Kibona, mmoja wa maelfu ya watu ninaowatumikia

Anakerwa na uamuzi wangu kupokea matangazo ya wenye uhitaji na kuyaweka hapa. Hanitendei haki kwa sababu kabla ya kuweka hapa ambapo hapazidi watu 2,000 huwa pia ninaposti Twitter ambako nina followers zaidi ya 120,000 na Instagram ambako nina followers zaidi ya 40,000.

Anatafsiri kuwa suala la mchango wa vijarida ni njaa yangu. As if kuwa na njaa ni dhambi. Ukiwa na njaa, kisha ukabuni njia ya kukabiliana nayo, unastahili pongezi, sio kebehi kama hizi.

Kama amekukera, basi usisite kumtumia ujumbe. Baruapepe yake ni essaukibona27@gmail.com au BONYEZA HAPA kumsaidia kiakili. Pia kama wamfahamu, nitaomba tuwasiliane nami faragha.

Vitu kama hivi vinavunja moyo lakini ni sehemu ya maisha

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali