Kama Ambavyo CCM Wanapelekeshana Na Gwajima, Ndivyo Chadema Wanavyoendeshana Mputa Na Kigogo

Yanayojiri CCM ambapo Mbunge wake wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima ameamua kumpinga Mama Samia Suluhu waziwazi kwenye suala la chanjo ya korona, ni mavuno ya upuuzi ambao chama hicho tawala umekuwa ukiufanya miaka nenda miaka rudi - kutumia dini kama mtaji wa kisiasa.

Na tabia hii haijaanza leo. Wakati wa harakati za kudai uhuru kutoka kwa wakoloni, TANU chini ya Mwalimu Julius Nyerere ilitegemea sana msaada wa Waislamu hasa wa mikoa ya Pwani, na msaada wao ulizaa matunda kwa uhuru kupatikana 09.12.1961.

Hata hivyo, uhusiano huo ulikuja kudhoofika, na mwaka 1968, taasisi muhimu kwa ustawi wa Waislam, ya East African muslim Welfare Society (EAMWS) ilipigwa marufuku na badala yake serikali ya TANU ikaanzisha BAKWATA, taasisi ambayo kwa takriban muda wote wa uhai wake, imekuwa ikitafsiriwa na idadi kubwa tu ya Waislamu kuwa ipo kwa maslahi ya serikali kuliko Waislamu wenyewe.

Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Jk na mtandao wake waliwatumia sana viongozi dini kuhakikisha mwanasiasa huyo anaingia Ikulu. Moja ya ahadi za mtandao wa Jk kwa Waislamu ilikuwa kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi pamoja na Tanzania kujiunga na OIC, lakini baada ya Jk kushinda, ahadi hizo zikapigwa teke, jambo ambalo wakati flani lilitishia kusababisha machafuko ya kidini.

Wakati kampeni za CCM kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 zilihusisha chama hicho kuomba msaada kwa jumuiya za kidini, ni utawala wa John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo ambao ulijenga mahusiano hatari kuliko yote kati ya chama hicho tawala na taasisi za dini.

Wakati taarifa zinaeleza kuwa viongozi wa ngazi za juu wa BAKWATA walikuwa “matabibu wa kiroho” wa Magufuli, kiongozi huyo aliwavuta viongozi wa makanisa mbalimbali, na kujenga uhusiano wa “nipe nikupe,” ambapo Magufuli aliwapatia sapoti mbalimbali viongozi hao ilhali nao walipita huku na kule kuwaaminisha Watanzania kuwa Magufuli ni chaguo la Mungu.

Ni mahusiano haya ndiyo yaliyomuibua Askofu Josephat Gwajima, na hatimaye kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Kawe, na kusaidiwa na Magufuli mwenyewe kuhakikisha anashinda ubunge. Hata hivyo, ahadi ya Magufuli kwa Gwajima kuwa angempa uwaziri haikutimia hadi kiongozi huyo alipofariki Machi 12 mwaka huu (serikali ilitangaza siku 5 baada ya mie mtumishi/jasusi wako ku-break news hiyo).

The rest is now history. What isn’t ni hicho kinachoendelea kati ya Mama Samia na wafuasi wake huko CCM dhidi ya Gwajima na genge lake. Nitaelezea kwa kina kuhusu suala hilo wakati mwingine.

Chadema nao, sijui kwa kuwa na ombwe la uongozi, walianzisha uhusiano na Kigogo, mtu anayefahamika zaidi kwa matusi kuliko hoja za msingi za kuweza kukisaidia chama hicho.

Mie jasusi wako, ambaye sio tu ni wahanga wa muda mrefu wa matusi ya Kigogo bali pia huniita “jasusi uchwara”, niliitahadharisha Chadema kuhusu uhusiano huo wa mashaka, lakini wakaweka pamba kwenye masikio.

Lakini kama ilivyotokea kwa Gwajima na CCM, ndoa kati ya Chadema na Kigogo sio tu imevunjika bali pia imeambatana na kutoleana maneno machafu.

Hata hivyo kabla ya kuwaletea baadhi ya twiti za ugomvi baina ya “maswahiba hao wa zamani” naomba niwarejeshe nyumba kidogo, na kuonyesha makala niliyoandika kuwatahadharisha Chadema.

Soma makala hiyo HAPA.

Na zifuatazo ni twiti mbalimbali kuhusiana na skata hilo