Jisajili Kupokea Kijitabu Hiki Bure Kila Mwezi

Ninakualika ujisajili kupokea kijitabu hiki cha kielektroniki cha bure ambacho nitakuwa nikikichapisha kila mwezi. Kijitabu hiki ni mkusanyiko wa twiti zangu zenye nukuu mbalimbali za motivation, inspiration, lifehacks, lifestyle, creativity na vitu kama hivyo ambavyo kwa pamoja vinaunda kitu kinachofahamika kama personal development, au kwa tafsiri isiyo rasmi, "jinsi ya kuwa mtu bora au kuboresha ubora wako."

Kila siku, kuanzia saa moja asubuhi ya hapa Uingereza hadi saa kumi na moja jioni, huwa ninabandika twiti moja kila saa, twiti inayohusu personal development. Nimekuwa nikifanya hivyo tangu mwezi Julai mwaka huu. Sasa kwa vile uhai wa twiti ni takriban dakika 18 tu nimeonelea ni vema kutengeneza kumbukumbu ya twiti hizo ambazo kwa mujibu wa mrejesho ninaopokea mara kwa mara, zinawasaidia watu wengi.

Toleo la kwanza lina twiti za mwezi Agosti, toleo la pili litakuwa na twiti za Septemba, la tatu Oktoba, na kuendelea.Ni twiti za personal development tu na sio masuala mengine.

JISAJILI HAPA ili kutumiwa kijitabu hiki

Kadhalika, yeyote ambaye hajapata nakala ya vitabu hivi hapa chini anafahamishwa kuwa bado vinapatikana.

Mwisho, yeyote anayejiskia kuwa mwanachama wa #BaruaYaChahali yenye mkusanyiko wa vijarida vinne kwa wiki, anaweza KUJIUNGA HAPA.

Na endapo usingependa kutumiwa baruapepe hizi kutoka kwangu, BONYEZA HAPA.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali