Barua Ya Chahali

Share this post
#JinsiYaKuwaMtuBora: Vitu Vinane Ambavyo Hujachelewa Kujifunza Maishani
www.baruayachahali.com
AdelPhil Online Academy

#JinsiYaKuwaMtuBora: Vitu Vinane Ambavyo Hujachelewa Kujifunza Maishani

Evarist Chahali
Jan 21
Share this post
#JinsiYaKuwaMtuBora: Vitu Vinane Ambavyo Hujachelewa Kujifunza Maishani
www.baruayachahali.com

Ufafanuzi kidogo. Kwenye masuala ya ujasusi, mie ni jasusi wako. Kwenye utumishi, mie ni mtumishi wako. Lakini kwenye haya masuala ya Jinsi ya Kuwa Mtu Bora aka “personal development” kwa kimombo, mie ni kocha wako. Kwanini “kocha”? Kwa sababu kuna fani inaitwa “ukocha wa maisha”, kwa kimombo “life coach.” Na hicho ndicho hasa nachofanya katika hizi kozi. Kwa muktadha huo, nawasilisha elimu hii kama KOCHA wako. Sio kocha wa soka au dhumna bali kocha wa maisha aka life coach.

Somo la leo linahusiana na kilio nachosikia kutoka kwa watu wengi kuhusu umri kuwatupa mkono. Kichekesho ni kwamba kuna vijana wadogo tu ambao hawajatimiza hata miaka 20 nao wanalalamika kuwa “umri umewatupa mkono.”

Pengine haipaswi kuwa kichekesho kwa sababu umri ni kitu cha kufikirika. Nadhani ushaskia msemo wa kimombo kuwa “age ain’t nothing but a number.” In fact, msemo huo ulipata umaarufu zaidi kufuatia kibao hiki cha marehemu Aaliyah. Burudika kidogo 😊

Twende kwenye somo husika.

Kitu kimoja kizuri kuhusu maisha ni kwamba haijaishi una umri gani, ukijibidiisha kupata ujuzi flani, basi maisha yatakuzawadia kitu hicho. Pengine neno sahihi zaidi sio ujuzi bali uelewa au funzo. Lakini nisichokonoe sana hapo, naamini umeelewa nini nachomaanisha.

Ukitaka mfano hao, mie kocha wako nina mifano “milioni kidogo.” Nadhani utakuwa unafahamu kuwa mie ni “mtu wa kujifunza angalau jambo moja kila siku.” Kwa maana hiyo, umri haujawahi kuwa kikwazo kwangu kujifunza vitu vipya, kwani kila siku ya maisha yangu ni sawa na kwenda darasani.

Moja ya vitu ambavyo nilijifunza ukubwani ni pamoja na matumizi ya kompyuta. Nilipokuja hapa UK miaka kadhaa iliyopita nilikuwa mbubumbu kabisa wa kutumia kompyuta. Lakini nilijifunza mwenyewe na sasa nimefikia kiwango cha kuwafundisha watu wengine sio tu matumizi ya kompyuta bali pia maeneo mengine muhimu kuhusiana na kompyuta kama vile usalama wa mtandaoni.

Na kadri navyozidi kuijua kompyuta ndivyo kadri navyopata kiu ya kujifunza vitu vingi zaidi. Mwaka 2018 nilianza rasmi safari ya kujifunza udukuzi wa kimaadili aka “ethical hacking,” japo kimsingi wazo la kozi hiyo lilitokana na ushauri wa rafiki yangu Erick Kabendera.

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
Asante sana #ErickKabendera (@kabsjourno). Ushauri wako umebaki kuwa moja ya misaada muhimu kabisa niliyowahi kupokea maishani. Maono yako kuwa "ujasusi + udukuzi wa kimaadili = marriage made in heaven" yametimia. Nakushukuru sana 🙏

Jasusi @Chahali

How it all started: bought the bundle in 2017 then I became lazy. Then early last year, #ErickKabendera (@kabsjourno) visited UK, and in our chat he advised, "would be a marriage made in heaven for an ex-spy to become an ethical hacker..." Thank you Erick, I'm nearly there now! https://t.co/EzTfVvrEkS

March 2nd 2021

2 Likes
Image

Ok, kuna vitu kadhaa hapa ambavyo sio ujuzi as such bali maisha yatakujalia kujifunza bila kujali umri wako.

Kuwa uncomfortable hakumaanishi upo sehemu isiyostahili: Kuna msemo wa Kiswahili kuwa kuku mgeni hakosi kamba mguuni. Moja ya maana zake ni kwamba hutoshindwa kumbaini mgeni. Pengine ni kwa kutojiamini kwake, pengine ni wasiwasi wake…na vitu kama hivyo. Mara nyingi ugeni kwenye sehemu au jambo flani huambatana na kuwa uncomfortable kwa namna flani.

Mfano hai kwangu ni kwamba nilipoanza safari ya ethical hacking, mara kadhaa nilijiuliza kama ni njia sahihi, hasa kutokana na ugumu kwenye maeneo flani. Ethical hacking inahitaji uelewa wa networks na mie nilikuwa mbumbumbu wa eneo hilo. So, mara kadhaa tu nilishawishika kuweka kando kozi hiyo na badala yake nianzie chini zaidi, au niachane kabisa na kozi hiyo.

Nawe utapoanza kitu kipya, kuna uwezekano wa kujisikia uncomfortable. Kuna uwezekano wa kujiuliza kama umechukua uamuzi sahihi.

Ali mradi ulitumia muda wa kutosha kutafakari kuhusu kitu husika, na ali mradi una mfumo wa kukusapoti (support system -hii inahitaji mada ya peke yake), basi utafanikiwa.

Kuwekeza kwako wewe mwenyewe hakuwezi kukuangusha: Mara nyingi tunatumia nguvu nyingi kuwekeza kwa wenzetu. Na kwa bahati mbaya kwa sie Waswahili, uwekezaji mkubwa zaidi hufanywa kwenye sekta ya anasa - hususan uzinzi.

Sasa sipo hapa kuhubiri maadili lakini ukweli mmoja ni kwamba kuwekeza kwenye anasa hakutozaa anasa zaidi bali majonzi. Kama ilivyo kwenye biashara, huwezi uwekezaji wa maana ni ule ambao sio tu utarudisha mtaji bali pia utatengeneza faida.

Anza leo kuwekeza kwako mwenyewe. Jielimishe. Jifunze ujuzi mpya. Anza kufolo watu wa maana mtandaoni badala ya kufukuzia ubuyu.Tafakari mahusiano yako na Mola wako. Kama inawezekana kuangalia “series” kila ski, kwanini ushindwe kusoma Biblia Takatifu au Korani Tukufu kila siku?

Kama unaweza kutokosa “kuhudhuria vikao kwenye viti virefu,” kwani ushindwe kufanya mazoezi japo mara moja kwa wiki?

Uzuri ni kwamba ukiwekeza kwako, lazima utavuna matunda tarajiwa.

Na kumbuka, kujijali sio ubinafsi. Na ili uweze kuwajali wengine, shurti ujijali mwenyewe kwanza.

Badala ya nyingi zijazo au zisizopo, angalia japo chache zilizopo: Mara nyingi watu wapo bize kulalamikia vitu ambavyo hawana. Na si kulalamikia tu, pengine vitu hivyo ndivyo vinawanyima usingizi. Wanachosahau ni ukweli kwamba kamwe katika maisha huwezi kuwa na cha kutosha. Ukipata mia utataka alfu, ukipata alfu utataka laki, ukipata laki utataka milioni, ukipata milioni utataka bilioni…na kadhalika na kadhalika.

Sasa anza leo kuangalia kidogo ulichonacho. Mshukuru Mungu kwa hicho kabla ya kumlalamikia kwanini hajakupa hiki au kile. Jipongeze kwa kufika hapo ulipo, kwa sababu kuna wengi tu wamefeli.

Haimaanishi ubweteke bali usiwe mtumwa wa “nyingi.”

Mie kocha wako huanza siku kwa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai. Na hii si ndogo kwangu kwa sababu nimenusurika majaribio kadhaa, na kwa miaka kadhaa sasa sitoki nje au kwenda sehemu au kufanya jambo bila kuhakikisha “nipo salama.” Na mara nyingi humaliza siku yangu kwa kumshukuru Mungu kwa kunilinda.

Huko mbeleni nitatoa darasa kuhusu “nguvu ya shukrani” (power of gratitude).

Usimsaidie mtu asiyehitaji kusaidiwa: Hili halihitaji maelezo marefu kwa sababu kujihangaisha kumsaidia mtu asiyehitaji kusaidiwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa: utapoteza muda wako na utaishia kumuudhi mbuzi.

تويتر \ Billy The GOAT على تويتر: ""Twing twang, twing twang"  https://t.co/BWjts5SqOg"

Kuwa peke yako ni bora kuliko kuwa kwenye kundi lisilo sahihi: Mie si muumini wa makundi. Yawe halisi au hayo ya mtandaoni. Na siku ukinion kwenye Whatsapp group, naomba uripoti kwamba mtu huyo ni feki. Simaanishi kwamba makundi hayo hayafai kwa asilimia 100 lakini kama unajali usalama wako mtandaoni, basi makundi hayo ni miongoni mwa sehemu za kuziepuka.

Mtaani nako, mara nyingi makundi huwafanya watu watende hata wasiyotaka ili tu wasiliangushe kundi. Lakini pia makundi hushawishi watu kuhusu vitu ambavyo pengine wasingependa kuvifanya. Makundi ya masuala ya ulevi, uzinzi, nk ni mfano mmojawapo.

Hapana, simaanishi kila kundi ni baya. SACCOS inayokusaidia kuongeza kipato sio kundi baya. Kundi la kujisomea vitabu pia si baya. Kundi la kiroho pia si baya. Hata kundi la kijamii - kuhamasisha mabadiliko, kutetea haki za wanajamii, nk - pia si makundi mabaya.

Lakini kumbuka kuwa mkombozi wako ni wewe mwenyewe, na hata kama makundi yanakusapoti, kimsingi upo peke yako. Na kuwa peke yako ni bora zaidi mara bilioni kuliko kuwepo kwenye kundi lisilofaa.

Na hii inahusu pia mahusiano baina ya watu wawili. Kuwa kwenye ndoa ambayo ni kama jela sio uvumilivu bali kutafuta kifo kwa presha bure. Na kumdeti mwenza anayekufanya utamani usingefahamiana nae, ni sawa na kuipelekea jela mwenyewe.

Binafsi, miongoni mwa nyakati bora kabisa maishani mwangu ni ninapokuwa peke yangu.

Adui yako mkubwa ni wewe mwenyewe. Na huyo pia ndio rafiki yako mkubwa: Hili halihitaji maelezo marefu.

Kwanza hakuna mtu anayeweza kukufanya ujisikie huna maana endapo wewe mwenyewe unaamini kuwa una maana.

Halafu hakuna mshindani mkubwa ambaye unapaswa kushindana nae kila siku zaidi yako wewe mwenyewe. Wewe wa leo unapaswa kuwa bora kuliko wewe wa jana, juzi,nk, na wewe wa kesho unapaswa kuwa bora zaidi ya wewe wa leo, na wa keshokutwa bora kuliko wa kesho. na kadhalika na kadhalika.

Ukijiona huna maana, utakuwa huna maana. Ukipenda utapendwa. Ukijitahmini utathaminiwa ilhali usipojithmani utapuuzwa.

Kila mtu yupo tofauti, ikiwa ni pamoja na wewe:

Ukienda insta, kuna jitihada kubwa ya kila mtu kuonekana tajiri sana. Au mwenye akili sana. Au anapendwa sana. Kama ni binti basi ni mrembo sana.

Na si insta tu, takriban kila mahala jamii inataka tuwe wa aina flani. Na wakati mwingine sio jamii as such bali ni akili yako tu inakuhunia.

Ukweli ni kwamba kila mtu yupo tofauti. Hata mapacha waliozaliwa kwa tofauti ya dakika tu wapo tofauti.

Badala ya kutaka kila mtu aiangalie dunia kwa mtazamo wako, jikite kwenye yanayokuhusu wewe mwenyewe. Ndio unataka katiba mpya, na ina umuhimu lakini heshimu maamuzi ya watu wengine, na mitazamo yao. After all, katiba inahusu HAKI na WAJIBU. Haki zako na za wenzako, na wajibu wako na wa wenzako.

Imani yako kuhusu jambo flani au dini yako sio lazima iwe ya kila mtu. Na kujaribu kulazimisha watu waamini sawa na wewe sio tu kunaweza kupelekea migogoro isiyo na lazima bali pia inaweza kukufanya ukafariki mapema kwa shinikizo la damu 😉

Unaweza kutengeneza maana yako mwenyewe ya “uzuri.” Kwa mzinzi, maisha mazuri ni kuwa na lundo la wenza wa kufanya nae uzinzi. Kwa mlevi, maisha mazuri ni kuwa na uhakika wa kinywaji kila siku. Kwa shabiki wa michezo, ni timu yake kushinda kila mara. Kwa wapenda mabadiliko ni kuona malengo yao yanatimia, malengo ambayo yanaweza kuangaliwa na dola kuwa ni uhaini.

Kwa kifupi, uzuri - wajambo lolote lile - unategemea zaidi mtazamo wako na imani yako. Au matakwa yako. Au usichokipenda. Wembamba au unene ni maamuzi binafsi. Huku nchi za Magharibi, kuwa fiti maana yake kuwa na mwembamba ilhali kwetu kitambi ndio dalili ya afya (na pesa? 😁). Well, afya haipimwi kwa mwonekano. Mtu anaweza kuwa mwembamba ilhali ana kansa, ilhali mwingine ni kibonge asiye na maradhi yoyote.

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
Mama naniliu: "Hehe, baba yake ana damu kali sana. Si unaona ametoa fotokopi kwa huyu mwanae ambaye amerithi hadi kitambi na kipara cha baba yake teh teh..." Me (kimoyomoyo): astaghafurillah. Kwashakoo hiyo! 😪
Gordon Ramsay Oh Dear GIF

September 6th 2020

8 Likes

Jumaa mubarak

OMBI: Kuwa balozi wa AdelPhil Online Academy kwa kuwaalika wenzio wajiunge kupata elimu inayoweza kusaidia kuifanya dunia kuwa mahala pazuri kuishi.

Share
Share this post
#JinsiYaKuwaMtuBora: Vitu Vinane Ambavyo Hujachelewa Kujifunza Maishani
www.baruayachahali.com
TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing