Je Wewe Ni Mhanga Wa Utawala Wa Rais Magufuli? Ulitimuliwa/Ulisimamishwa Kazi/Ulikamatwa/Ulifungwa/Uliporwa/Ulidhalilishwa/Ulihujumiwa Kionevu? Ndugu/Jamaa/Rafiki Alitekwa/Aliteswa/Aliuawa?

Projekti ya HAKI ZA WATU inakusanya taarifa kuhusu ukiukwaji wa haki mbalimbali za Watanzania, na hata wasio Watanzania, zilizofanywa na utawala wa marehemu John Magufuli tangu alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 hadi alipofariki Machi 12, 2021 (japo serikali ilitangaza kifo hicho Machi 17, 2021).

Taarifa husika zitashughulikiwa kwa usiri mkubwa.

Pamoja na sababu nyingine, lengo la kukusanya taarifa hizo ni kuhakikisha kuwa ukiukwaji wa haki mbalimbali uliofanywa katika kipindi hicho haurudiwi tena. Kadhalika, projekti hii itawasiliana na wanasheria wa kitaifa na kimataifa endapo mhusika ataafiki, ili kusaka haki ikiwa ni pamoja na fidia.

Huduma hii ni ya bure, na mhusika hatotakiwa kugharamia chochote.

Kwa taarifa zaidi, BONYEZA HAPA