Janga La Musiba

Katika toleo la wiki hii la #BaruaYaShushushu, jasusi wako ninaingia kwa kina kwa mtazamo wa kiintelijensia kuweleza wanachama wa kijarida hicho za janga linalozidi kushamiri, la mtu hatari kuliko virusi vya Ebola, Musiba.

Nimelazimika kukalia kitako suala hili kwa sababu mbinu anazotumia sasa ni za hatari kuliko wakati mwingine wowote ule.

Mtumishi wako nilikuwa mhanga wa uhuni wake hivi majuzi ambapo akaunti yangu ya Twitter ilifanyiwa kitu kinaitwa ‘cloning,’ kisha wakai-photoshop na kuweka maneno machafu. Bahati nzuri jitihada zao zikaishia miononi mwao tu - yahitaji uelewa mkubwa wa social media ili uweze kufanya kitu (mfano tweet/picha) kiwe “viral” (kisambae kwa wingi).

Anyway, ni hapo kesho. Kama hujajiunga kuwa mwanachama, waweza kufanya hivyo kwa kufuata maelezo haya hapa chini

Uanachama kwa mwaka mzima ni sh100,00 au sh 10,000 kwa mwezi. Tuma mchango wako kwa m-pesa namba 0767632516 (jina Khadija Katule). Kwa walio nje ya Tanzania, unaweza kuchangia kwa KUBONYEZA HAPA.

Ndimi jasusi wako,

Evarist Chahali