Janga la #Coronavirus Tanzania: Yu Wapi 'Rais wa Wanyonge' Magufuli?
Makala hii inaamsha tafakuri kuhusu kasumba iliyozoeleka ya Rais Magufuli “kurudi nyuma” kila linapojitokeza janga katika Tanzania yetu. Tulishuhudia hilo wakati wa tetemeko la ardhi huko Kagera, tulipopoteza mashujaa wetu waliouawa wakati wakilinda amani huko DRC, janga la vifo vya watoto wa shule kule Arusha, na matukio mengine kadhaa.