In Defence of both Mheshimiwa Zitto Kabwe Na Waziri January Makamba

Jana nilikumbana na bandiko flani huko Jamii Forums ambalo nilipelekea niwasiliane na ma-admin wa jukwaa hili la kijamii kuwasihi wachukue hatua stahili dhidi ya udhalilishaji uliokuwemo kwenye bandiko husika.

Hii ni moja ya comments kwenye bandiko hilo, sintoweka nyingine kwa sababu nitakuwa “nampiga chura teke.”

Cha kusikitisha ni kwamba licha ya kuwepo kitufe cha kuripoti bandiko linalokiuka maadili ya jukwaa hilo, ilichukua kitambo kabla ya hatua stahili (kuondoa comments husika) kuchukuliwa. Unfortunately, kila sekunde ya udhalilishaji kubaki mtandaoni kuna madhara yasiyorekebishika hata kama bandiko husika litafutwa.

Hata hivyo, naomba nitanabaishe mapema kuwa siilaumu Jamii Forums, jukwaa ambalo nimekuwa mwanachama kwa takriban miaka 15 sasa. Siilaumu kwa sababu dhamira ya jukwaa hili sio tu ni nzuri bali imekuwa na msaada mkubwa kwa Watanzania hususan katika mazingira ya kubinya uhuru wa habari.

Kwangu, mmoja wa mashujaa muhimu wa Tanzania yetu ni mwasisi wa mtandao huo, Maxence Mello, ambaye licha ya changamoto lukuki alizokumbana nazo, ameendelea kuiweka Jamii Forums kuwa jukwaa muhimu la mijadala miongoni mwa Watanzania.

Changamoto kwa jukwaa hilo ni (a) watumiaji ambao kila mada inapaswa kuangalia kwa lensi ya “u-CCM” au “u-Chadema.” Japo ni haki yao, lakini msimamo huo unakwaza mijadala yenye manufaa, kwa sababu kwao ni “my way or no way.” (b) watumiaji wenye majina feki wanayoyatumia kama silaha na kinga ya kuchafua/kudhalilisha watu wengine. Ikumbukwe lengo la kuficha jina halisi ni zuri (kwa mfano mtumiaji anapotaka kufanya “whistleblowing”) lakini tatizo ni pale kuficha jina huko kunapowapa baadhi ya watumiaji ujasiri wa kuchafua/kudhalilisha wenzao kwa vile wanaamini kuwa “hakuna anayenifahamu.”

Wito wangu kwa Jamii Forums ni kuhamasisha watu wengi wapate ujasiri wa kutumia majina yao halisi, ilhali kwa wenzetu watakaoamua kubaki anonymous basi iwe si kwa ajili ya kunyanyasa watumiaji wengine.

Niende kwenye mada husika. Na nianze hapo kwenye tuhuma za “Kigogo ni Zitto, Chahali…” Mmoja wa waasisi wakuu wa uzushi huu ni Yeriko Nyerere.

Na hii si mara ya kwanza kwa Yeriko kunifanyia uzushi. Huko nyuma alipelekea nitukanwe na Mange baada ya jitihada zake kuaminisha umma kuwa mie ndio mtu anayejiita Daudi Balali huko Twitter kudakwa na haramia Musiba

Moja ya mafanikio makubwa sana ya Magufuli yalikuwa kuweza kuwafarakanisha watu waliopaswa kushikamana kupambana na udikteta wake. Na mbegu aliyopanda itadumu milele unless wenzetu walioingia mkenge na kuanza kututukana watapatwa na ujasiri wa kututaka radhi. I know that’s not going to happen lakini hakuna ubaya kumshauri mtu afanye kitu sahihi.

Kumtuhumu Mheshimiwa Zitto kuwa ni Kigogo sio tu ni kupotosha ukweli bali ni kumdhalilisha mwanasiasa huyo. Natanabaisha hivyo kwa sababu mie ninamfahamu Mheshimiwa Zitto tangu akiwa mwanafunzi UDSM, na mie wakati huo nikiwa Afisa huko Kitengoni. Zitto aliwasumbua sana watu wa Kitengo kwa sababu silaha yao kubwa ya kutisha watu wenye msimamo thabiti ilifeli kwa mwanaharakati huyo (wakati huo Mheshimiwa Zitto alikuwa mwanaharakati kabla ya kuwa mwanasiasa kamili).

Moja ya mambo makubwa kabisa ambayo Mheshimiwa Zitto ameyafanya kwa Tanzania yetu ni jitihada zake za kila mwaka, kwa miaka kadhaa sasa, kutufanyia uchambuzi wa kina wa taarifa mbili muhimu kabisa kwa nchi yetu, namely ripoti ya CAG na hotuba ya bajeti.

Kwa sababu wanazojua wenyewe, ripoti ya CAG sio rahisi kueleweka, kama ilivyo hotuba ya bajeti. Kwanza ni ndefu mno, lakini pili lugha inayotumika kwenye machapisho yote mawili ni ya kitaalamu zaidi. Na Mheshimiwa Zitto amekuwa akichukua muda wake kutuchambulia na kisha kuwasilisha kwa lugha rahisi kueleweka. Bila yeye, hotuba hizo zingeishia kusalaulika pasi Watanzania wengi kuelewa undani wa yaliyomo.

Lakini pia, akiwa Chadema, Mheshimiwa Zitto aliwezesha uwepo wa “utatu mtakatifu wa siasa za Tanzania,” yeye, Mheshimiwa Mbowe na Dokta Slaa. Pengine Watanzania wengi watakuwa hawaelewi kazi kubwa iliyofanywa na “utatu huo mtakatifu” hasa kwa vile zama hizo, baadhi ya mitandao ya kijamii, kama vile Instagram, ilikuwa haijazaliwa.

Kadhalika, hata huko Twitter, tulikuwepo Watanzania wachache tu, ilhali matumizi ya Whatsapp yalianza kushika kasi baadaye zaidi. Kwahiyo kwa kifupi, upashanaji habari haukuwa rahisi sana. Lakini kwa vile Watanzania wengi wana “allergy” na historia ya Tanzania yetu, si ajabu kuona wengi wao hawafahamu vizuri mchango mkubwa wa “utatu huo mtakatifu wa kisiasa” ambao pamoja na mafanikio yake makubwa ilikuwa kuchapisha LIST OF SHAME (ambayo kwa sababu wanazojua Chadema pekee, iliondolewa kwenye tovuti yao kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015)

Makala hii haitoshi kueleza mchango mkubwa wa Mheshimiwa Zitto kwa Tanzania yetu, lakini moja ambalo pengine mwenyewe hatopendezwa niliandike ni mchango wake mkubwa kabisa kuepusha balaa lililokuwa litokee kufuatia kuugua na hatimaye kufariki kwa Magufuli.

Mheshimiwa Zitto alifanya jitihada kubwa mno behind the scene kuhakikisha kuwa mipango yote dhalimu dhidi ya utaratibu wa kikatiba kufuatia kuugua na hatimaye kufariki kwa Magufuli unafuatwa. Yayumkinika kutanaiabaisha bila shaka kuwa pasipo jitihada binafsi za Mheshimiwa Zitto, huenda nchi ingekuwa kwenye mahafuko muda huu kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na maharamia kadhaa kujaribu kunajisi katiba ili izuwie smooth transition of power to Mama Samia.

Wanaosema Mheshimiwa Zitto ni “mmoja wa watu wanaounda jitu linalojiita Kigogo” wanajifanya vipofu kwamba hawakuona kuwa Mheshimiwa Zitto, kama nilivyo mie mtumishi wako, alikuwa mmoja wa wahanga wa takriban kila siku wa “bingwa wa matusi.” Na kabla Kigogo hajapokea kijiti kutoka kwa Musiba, Mheshimiwa Zitto aliongelewa kila baya na toilet papers za Musiba, kiasi kwamba kuna wakati nilimtumia DM kumtaka achukue hatua hdidi ya haramia huyo lakini akanijibu kistaarabu kuwa “mwache tu aongee.”

Kwa upande wa Waziri January Makamba, nadhani makala hii inajitosheleza “kumtetea” dhidi ya lawama mbalimbali zinazoelekezwa kwake kuhusiana na changamoto za umeme.

Kinachomponza Waziri January, na Mheshimiwa Zitto, pia, ni kwamba “kwa mujibu wa siasa za sasa, haipaswi wawili hao kuwa na mahusiano mazuri.” Kwahiyo Mheshimiwa Zitto akisimamia kwenye ukweli, kama ilivyo kawaida yake, na kutanabaisha changamoto zinazoikabili Tanesco na sekta ya umeme kwa ujumla, inatafsiriwa kuwa “ana maslahi binafsi” kama sio “yeye ni mpiga debe wa January” au “ ni kuwadi wa mafisadi wa sekta ya umeme.” It hurts a lot kuona decent people wanachafuliwa kwa vile tu wanasimamia ukweli.

Lakini kwa upande mwingine, both Waziri January na Mheshimiwa Zitto ni easy targets kwa, on one side, wapenda ubuyu, and on the other, wapinzani wao wa siasa. Kwa wapenda ubuyu, wanasiasa wawili wenye mvuto mkubwa katika siasa za Tanzania, yaani Waziri January na Mheshimiwa Zitto, wanatengeneza perfect target kwa stori za kizushi. Na ndio maana uzushi dhidi ya wanasiasa hao kisiasa, huambatana na uzushi mwingine kuhusu maisha yao binafsi.

Kwa mahasimu wao kisiasa, ukaribu wa aina yoyote kati ya Waziri January na Mheshimiwa Zitto unawanyima watu wengi amani. Waziri January ni mmoja wa wanasiasa adimu ndani ya CCM wasioendekeza siasa za uhasama. Na Mheshimiwa Zitto, licha ya misimamo yake dhabiti dhidi ya CCM, ni mwepesi wa kusoma mazingira na kuwa tayari “kukaa kitako” na CCM kwa maslahi ya nchi. Wengi hamuwezi kuelewa hili lakini hata kwenye ujasusi kuna nyakati tunalazimika kukaa kitako na maadui zetu ili kusaka ufumbuzi.

Ukaribu huo wa wanasiasa hawa unatazamwa kama unaoweza kujenga “umoja wa kitaifa kwa Tanzania Bara” kati ya CCM na ACT-Wazalendo. Kwa bahati mbaya, hili linazua upinzani sio tu ndani ya CCM bali hata miongoni mwa vyama vya upinzani.

Nihitimishe kwa kutanabaisha kuwa sijatumwa na mtu yeyote kuwatetea wanasiasa hao wawili. Nimefanya hivyo ili kuweka rekodi sawia. Taifa letu linakabiliwa na upungufu mkubwa wa uwekaji rekodi sawia, no wonder ni watu wachache tu wanafahamu kwa hakika nini kilikwamisha itikadi ya Ujamaa, Azimio la Zanzibar lililozika tikadi ya Ujamaa ni nini hasa, kifo cha Sokoine kilitokeaje, na hata “ilikuwaje mwanasiasa asiye na jina kama Magufuli kuweza kushinda mchakato wa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015.” Ili kuyajua hayo kunahitajika watu wa kuweka rekodi sawia. Unfortunately, watu wengi wapo bize kwenye kuweka rekodi ya Daimond katika nani, au kweli Reivani kaachan na Paula Kajala. UBUYU NI JANGA LA KITAIFA.

Wikiendi njema.

Usisahau kujisajili na jarida la Ujasusi