Idara ya Usalama wa Taifa acheni uzembe, mnamuangusha Mama @SuluhuSamia, kama mnafeli kwenye vetting za ma-DC, mtaweza kweli kukabili changamoto kubwa kama kukabiliana na ugaidi?
Kwa mara nyingine tena - sijui mara ya ngapi sasa - uzembe uliofanywa na Idara ya Usalama wa Taifa umesababisha kituko ambapo baadhi ya ma-DC walioteuliwa na Rais Samia Suluhu hivi majuzi, wamegomea teuzi hizo.
Wakati ni rahisi kudhani kuwa wateuliwa hao wamekosa nidhamu kwa mkuu wa nchi, ukweli ni kwamba kiutaratibu, kabla Rais hajateua mtu huwa anapele…