Huku Jiwe Akificha Ripoti ya CAG, Mwanae Bashite Amnyanyapaa Pierre

Tukio lililotawala zaidi katika majadiliano mbalimbali katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ni kitendo cha Daudi Albert Bashite kunyanyapaa “Pierre Mzee wa Likwidi.”

Bila haja ya kuingia ndani sana kwenye suala hilo kwani tayari limeshaongelewa vya kutosha, tatizo sio ujumbe bali mtoa ujumbe. Alochoongea Bashite kina mantiki, lakini tatizo yeye kama haramia hatari kabisa kuwahi kutokea nchini Tanzania sio mtu sahihi wa kuongelea maadili.

Ofkoz, Tanzania yetu ina tatizo la kuwatukuza watu wa ovyo. Unamkumbuka Babu Ambi?

Image result for magufuli kikombe cha babu

Unamkumbuka Dokta Shika?

Image result for dokta shika

Wakati Babu Ambi alivuma kwa utapeli wa “tiba ya kikombe” ambayo miongoni mwa walioingizwa mkenge ni Jiwe kama anavyoonekana pichani, Dokta Shika alivuma kutokana na porojo kuwa ni bilionea flani. Ni rahisi sana kuwahadaa Watanzania kwa sababu asilimia kubwa ya Watanzania ni wavivu wa kujiridhisha iwapo kitu ni cha kweli au cha uongo. Ni wahanga “readymade” wa fake news.

Kwa upande wa Pierre, umaarufu wake unatokana na mwonekano wake sambamba na ulevi wake.

Bila kuuma maneno, Pierre sio role model. Huko kuonekana na kinywaji muda wote sio kitu cha kuvutia sana kwa watoto/vijana kwa sababu ulevi ni adui wa maendeleo, na hilo halia mjadala. Lakini pia ulevi una atahri kiafya, ambapo mywaji wa bia kila siku ana uwezekano mkubwa wa kupata kisukari cha aina ya pili (Type 2 Diabetes).

Kama nilivyotanabaisha awali, “kosa2 la Bashite sio kumkemea Pierre bali yeye kama Bashite hana uhalali wowote wa kumuongelea “mlevi” huyo. Katika logic nyepesi tu, “ulevi” wa Pierre hauwezi kulinganishwa na ujahili mkubwa kabisa wa Bashite. Pierre ahajawahi kumuumiza mtu - labda kuumiza tu mbavu za anaowachekesha - ilhali orodha ya watu wahanga wa Bashite ni ndefu kuliko reli ya SGR.

Lakini kwa upande mwingine, mkasa huo wa Bashite unaweza kunsaidia kutambua jinsi gani anavyochukiwa, kwa sababu ameshutumiwa mfululizo kila kona.

Lakini wakati macho na masikio ya Watanzania yakielekezwa kwa Bashite, baba yake Jiwe amaefanya kituko cha karne. Tofauti na utaratibu uliozoeleka wa ripoti ya CAG kupokelewa hadharani, safari hii ripoti hiyo imepokelewa kimyakimya

Wakati Watanzania wana hasira dhidi ya mwanae Bashite kwa kumnyanyapaa Pierre, hakujasikika kelele zozote za maana dhidi ya kitendo hiki cha Jiwe. Unaweza kusema kwani tatizo lipo wapi? Tatizo lipo kwenye ukweli kwamba ripoti iliyopoita ya CAG iliibua ufisadi wa SHILINGI TRILIONI 2.4

Ni wazi kuwa ripoti ya CAG inafichwa kwa sababu kuna uwezekano wa kuwepo ufisadi mkubwa zaidi ya huo wa trilioni 2.4. Kwa bahati mbaya - au makusudi - ishu hiyo ndio imetoka. Watanzania wapo bize na UBUYU na hakuna uwezekano wa kuwepo shinikizo kudai ripoti hiyo iwekwe hadharani.

Naomba kutumia fursa hii kuomba yeyote anayewexza kupata nakala au hata muhtasari wa ripoti hiyo anitumie ili nami niwashirikishe Watanzania wengi zaidi. Jiwe hapaswi kuificha ripoti hiyo kwa sababu inahusu pesa zenu nyie walipakodi.

Lakini ishu hii ya Jiwe kuficha ripoti ya CAG inaweza kuturejesha tena kwenye kauli ya Bashite kuhusu “vitu vya ovyo ovyo.” Hivi kati ya suala la yeye Bashite na Pierre na hili la kihistoria la “ripoti ya CAG kupokelewa kinyemela,” lipi lililopaswa kuwakera zaidi Watanzania? Simaanishi kuwa ni sawa kwa Bashite kumnyanyapaa Pierre lakini nadhani ishu ya CAG ina umuhimu mkubwa zaidi.

Nakutaki April njema. Tukutane Jumatatu ijayo.

Mtumishi wako Evarist Chahali