Habari njema kwa Watanzania kuhusiana na muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaotarajiwa kupitishwa leo huko Bungeni
Kwa mujibu wa ratiba za bunge, muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa 2023, itajadiliwa leo, na inatarajiwa kupitishwa bila kipingamizi licha ya kuwepo kwa maeneo kadhaa yanayotishia haki za kiraia.
Kwamba muswada huo utapitishwa kirahisi wala sio suala la kuhoji kwa sababu wabunge wa chama tawala CCM wana kazi moja tu ya kuwa mhuri kwa kila kinacholetwa bungeni na serikali.
Lakini pia kumekuwa na taarifa za vitisho dhidi ya yeyote yule atakayejaribu kukwamisha muswada huo ulioletwa bungeni kwa hati ya dharura.
Kama hujausoma muswada huo, upitie hapa chini pamoja na uchambuzi mfupi kuhusiana nao
Hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba “Tanzania baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo haitokuwa the same”, kuna habari njema.