Guest Column: Ushauri Kwako Mama Samia Kutoka Kwa Kada Wa Chama Chako CCM Kuhusu Masuala Mbalimbali

Kijarida hiki ambacho kimsingi ni chenu Watanzania, nami ni mtumishi mwendeshaji tu, sasa kinapokea makala kutoka kwa wadau mbalimbali. Endapo kutahitajika uhariri, basi nifahamishe mtumishi wako.

Katika toleo hili, kuna makala ya kada mmoja wa CCM ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe. Anatoa ushauri kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Rais Mama Samia Suluhu.

Mwaka 2015 niliandika maoni yangu kwenye mitandao ya kijamii kumshauri Hayati JPM mara baada ya kuapishwa kushika nafasi ya Urais wa Tanzania. Bahati haikuwa nzuri kwa sababu mengi niliyoyatolea angalizo yalitokea na hatimaye kumuweka kwenye mtafaruku wa kisiasa.

Pamoja na kelele zinazopigwa hapa na pale lakini haiondoi ukweli kwamba wewe ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa majenzi ya Ulinzi na Usalama.

Umeanza kwa hatua nzuri sana tena zinazoacha bumbuwazi kwa wanaotarajia kuwa hautaweza kuitendea haki nafasi ulitoapishwa kuitumikia.

Nina machache mno ya kukushauri ingawa yanaweza kuonekana ya kijinga lakini unaweza kuyaangalia kwa jicho tofauti zaidi.

1. WASHAURI

Kuwa muangalifu na washauri wako gawa wa upande wa Siasa na Jamii. Hawa mara nyingi hupenda kujibadilisha na kuwa kingmakers.

Utaletewa majina ya uteuzi kwa nafasi mbalimbali, unaweza kuletewa na vertings zilizosheheni mbwembwe nyingi na produces facts lakini kumbe behind ya scene ni kukupelekea ufanye political blunders.

Wateule wa sasa ambao tayari wameshaonesha makandokando waweke pembeni weka watu wanaoendana na falsafa yako ya kuifungua nchi. Hawa waliopo unawajua na walitumika sana kuibana na kuifunga nchi ili kufanikisha malengo waliyopangiwa.

Kwenye teuzi unazozifanya, jitahidi kwenda mbele zaidi ya vetting kwani kuna wakati wanaofanya vetting ya wateule wanaweka malengo ya kimkakati kukupatia taarifa zinazoweza kupindisha matarajio ya serikali yako.

2. UCHUMI

Vitambulisho vya Wajasiriamali ni incubator ya uchumi kwa wafanyabiashara wa chini waweze kupanda viwango. Ukiviboresha na kuviwekea details zinazompa uhalali anatekikata kuaminika kwenye microfinances irasaidia sana mzunguko wa uchumi kwa madaraja yote.

Iangalie Tanzania Chambers of Commerce kwa uangalifu sana. Ujiulize kwa nini uwiano wa uwekezaji wa Watanzania nje na wageni wanaowekeza kwetu hauko fair?

A. Fair Trade

Tanzania iliridhia mkataba wa Fair Trade kupitia WTO lakini hakuna juhudi za watendaji wako kuwaunganisha Watanzania kwenye soko hili kubwa ulimwenguni ambalo limeiinua sana Asia. Biadhaa nyingi za majirani zetu Wakenya ziinazopelekwa Fair Trade zinatoka hapa kwetu na wanaziwekea brand ya Kenya hivyo tunarudi kwenye story ya Tanzanite..

B. AGOA

Hii opportunity imetwaliwa na Wachina kupitia viwanda vya uwekezaji Ethiopia, Kenya na Zambia. Nafasi ingalipo na tunaweza kuliingia kwa kasi kubwa

C. REGIONAL TRADE

Hapa uangalie korido za SADC, EAC, EPA na mengineyo. Tunapofungua fursa kwa wawekezaji kutoka nje, je uwiano wa sisi kuwekeza huko kwao upoje? Je vigezo ni parallel au competetive?

D. TRADE INTEL

Hatuwezi kama Tanzania kufika mbele bila kuwa na ukusanyani na uchakataji wa taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia watu wetu kuwekeza maeneo ya nje yenye fursa.

AEGIS ni shirika binafsi lakini lina mkono wa serikali ya Uingereza ambalo kazi yao kubwa ni kuangalia, kulinda na kutafiti kwa maslahi ya wawekezaji wa Uingereza na baadhi ya sehemu ya Ulaya.

CIA inafanya ujasusi wenye maslahi ya kiuchumi kwa nchi ya Marekani.

Sisi siyo kisiwa,ni muhimu tuwe na kurugenzi au taasisi inayojitegemea inatofanya ujasusi wenye maslahi ya Tanzania kibiashara

3. ULINZI NA USALAMA

Wewe na mtangulizi wako mliiweka nchi yetu salama kabisa. Lakini haiondoi ukweli kwamba bado zipo chokochoko hususani jirani na mpaka wa Msumbiji, mpaka wa magharibi na kaskazini.

Ni vizuri ukaiangalia TAMISEMI hasa nafasi za viongozi wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa wapewe uwezo zaidi kwenye eneo hilo kusaidia kuiweka salama chini yetu.

5. SIASA

Mheshimiwa Rais, ruhusu vyama vya siasa vifanye shughuli zao. Tekeleza ahadi yako ya serikali mseto kusaidia kuiponya nchi.

Kuwa muangalifu sana na washauri wa Siasa. Ninairejea hii kauli kwa tahadhari kubwa sana. Wanachama wengi wa CCM wapo kimya wakiangalia kinachoendelea ndani ya Serikali yako. WanaCCM wengine ambao wengi wao walikuwa mstari wa mbele kuwararua kwa hoja kali wale wote waliojaribu kukosoa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Kisiasa umeanza na turufu nzuri sana ya kupendwa na kukubalika na watanzania aina zote yaani wanaoisapoti CCM na wale walioipinga CCM kwa nguvu zote.

Mwandishi ni mwanachama hai wa CCM