Barua Ya Chahali

Share this post
Free Access: What's next baada ya Mahakama Kuu kusema Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu?
www.baruayachahali.com

Free Access: What's next baada ya Mahakama Kuu kusema Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu?

In less than 48 hours tangu Lissu akutane na Mama Samia, ndoto za "mwafaka" zinaelekea kufa kwa kasi baada ya uamuzi wa Jaji Tiganga kufuatia "mvua ya maneno makali" ya wana-CDM dhidi ya Mama Samia

Evarist Chahali
Feb 19
2
Share this post
Free Access: What's next baada ya Mahakama Kuu kusema Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu?
www.baruayachahali.com

ANGALIZO: Endapo makala hii “itakatikia njiani kwenye email yako” basi soma makala tovutini HAPA

Jana, Jaji Joachim Tiganga, alitoa uamuzi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na wenzake watatu, ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi na uhujumu wa uchumi.

Uamuzi huo uliokuwa ukisbiriwa kwa hamu ulihusu endapo Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu au la, kufuatia upande wa mashtaka kukamilisha kuwasilisha ushahidi wake.

Mazingira kabla ya uamuzi huo

Kwa wana-Chadema wengi, uamuzi uliotarajiwa ni “no case to answer.” Na katika kuthibitisha hilo, baadhi ya wanachama wake walichapisha fulana zenye maneno hayo.

Sijui confidence hii ilitoka wapi

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
Kama all along kesi iliitwa "kesi ya mchongo," na jaji Tiganga nae akaitwa "jaji wa mchongo," sasa haya matumaini ya "no case to answer"👇 yalitoka wapi? 🤔
Image

February 18th 2022

5 Retweets55 Likes

Japo Chadema hawatopenda kusikia hili, lakini moja ya changamoto zinazokikabili chama hicho ni pamoja na chama hicho kuzidi kuonekana kama kundi la harakati badala ya chama cha siasa.

Kuandaa fulana na hashtag za “no case to answer” badala ya kuwa na mikakati kuhusu nini kifanyike endapo Jaji Tiganga atafanya uonevu, ni uthibitisho kuwa chama hicho kwa sasa ni kama kundi la harakati.

Mkutano kati ya Mama Samia na Tundu Lissu

Kuna waliotumaini kuwa mahakama ingewaona Mbowe na wenzake kuwa hawana kesi ya kujibu, kutokana na mkutano wa Jumatano kati ya Mama Samia na Lissu, huko Ubelgiji.

Ikadhaniwa kwamba maombi ya Lissu kwa Mama Samia kushughulikia kesi hiyo yangepelea Mbowe na wenzake kukutwa hawana kesi ya kujibu. Haikuwa hivyo.

Hata hivyo kuna imani kuwa Mama Samia atachukua hatua stahili kumaliza kadhia hiyo. Lakini ili hilo litokee itakuwa lazima kwa Chadema kuwa wastaarabu na kuacha kumkebehi, kumtukana na kumdhalilisha Mama Samia.

Miongoni mwa “hatua muhimu” zilizochukuliwa na wafuasi wengi wa chama hicho baada ya Jaji Tiganga kutangaza uamuzi wake kuwa Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu, ni kumvurumishia Mama Samia takriban kila neno baya unaloweza kulifikiria.

Na neno moja lililojirudia sana ni “Samia ni dikteta” huku wengine “wakimfananisha na Magufuli.”

Twitter avatar for @IAMartin_Martin Maranja Masese @IAMartin_
Image

February 18th 2022

136 Retweets1,534 Likes

Lakini hakuna cha kushangaza hapo. Kwa wanaofutailia mwendo wa chama hicho watakumbuka vema walivyosimama kidete na Didier Abdallah Mlawa aka Kigogo alipomtukana Mama Samia matusi ya nguoni.

Barua Ya Chahali
[Tahadhari Ya Matusi Ya Nguoni] Huu Sio Unaharakati, Haya Ni Matusi Na Udhalilishaji Dhidi Ya Mama Samia.
“Kushindwa kuonya ni dhambi kubwa kabisa katika taaluma ya intelijensia.” Naam, sisi ambao bado tunaendelea kuwa wadau wa taaluma hiyo (hadi tunaingia kaburini) tunawajibika kuepuka dhambi hiyo. Pia ni muhimu kwetu (maafisa wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa) kutimiza wajibu huu kutokana na ukweli kwamba Idara yetu ya Usalama wa Taifa ipo hoi bin taa…
Read more
a year ago · 1 like · Evarist Chahali

Na kijarida hiki kilikuwa chapisho pekee mtandaoni kutahadharisha kuhusu mrengo mpya wa chama hicho. Kwa upande mmoja, uswahiba wao na “wanaharakati wa mtandaoni.”

Barua Ya Chahali
Uswahiba Wa Chadema Na "Wanaharakati wa Mtandaoni" Na Mustakabali Wa Chama Hicho
Nianze makala hii kwa kutanabaisha mapema kwamba mimi sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa tangu mwaka 1995 nilipojiunga na utumishi serikalini. Kuanzia hapo sheria ilinikataza kujihusisha na siasa isipokuwa pale tu majukumu ya kikazi yalihitaji iwe hivyo…
Read more
a year ago · 3 likes · Evarist Chahali

Na pia jitihada endelevu na za makusudi “kumlazimisha Mama Samia awe kama mtangulizi wake.”

Barua Ya Chahali
Onyo Kuhusu Chokochoko: Kuna Wanaojitahidi Kumlazimisha Mama Samia Awe Mbabe Kama Mtangulizi Wake
Read more
10 months ago · Evarist Chahali

Tarehe 19 mwezi ujao, Mama Samia atatimiza mwaka kamili tangu aapishe kuwa Rais wa sita wa Tanzania. Kutakuwa na chambuzi mbalimbali kuhusu utawala wake katika kipindi hicho. Lakini pia inaweza kuwa fursa muhimu kwa Chadema kujitathimini kwenye “approach” yao katika ku-engage na Mama Samia.

Yeyote anayefuatilia vizuri siasa za Tanzania hatoshindwa kutambua kuwa Mama Samia alionyesha dhamira ya dhati ya kujenga upya, kuboresha na kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa, sambamba na kuchukua hatua za makusudi - ambazo zingeweza kugharimu uhai wake wa kisiasa ndani ya chama chake cha kihafidhina CCM - kuondokana na mapungufu mbalimbali ya mtangulizi wake.

Lakini pia kwa yeyote anayefuatilia vizuri siasa za Tanzania hatoshindwa kubaini kuwa tangu Mama Samia aningie madarakani, Chadema walikuwa kama wanataka kum-patronise. Baada ya kutamka kuwa angekutana na viongozi wa upinzani, wakaanza “kumuwashia moto” kushinikiza mkutano huo. Sasa huhitaji kuwa na busara kubwa kutambua kuwa kiongozi hukumbushwa kistaarabu na sio kwa shinikizo hususan katika suala ambalo utashi wake tu umemtuma kulifanya.

Naam, pengine kwa uzembe au kutojua, viongozi na wafuasi wa Chadema wamekuwa wakipuuzi ukweli kwamba japo uongozi wa nchi unapaswa kuzingatia Katiba, kwa kiasi kikubwa tu -na hii si Tanzania pekee - utashi binafsi wa kiongozi husika una umuhimu mkubwa mno.

Mama Samia aliposema angekutana na wapinzani, alikuwa anafahamu kabisa kuwa hata angesema “kamwe sintokutana na wapinzani” asingekumbwa na athari yoyote ile. Mfano hai ni jinsi Magufuli “alivyowapelekesha” wapinzani kwa miaka mitano mfululizo lakini hakuna hatua yoyote ya maana iliyochukuliwa sio tu na “mabeberu” bali hata hao waliokuwa wahanga wake.

Matarajio kuwa mkutano kati ya Lissu na Mama Samia ungeleta mwafaka yanaelekea kufa less that 48 hours tangu viongozi hao wakutane

Yes. Unfortunately. Lakini hili sio la kushangaza kwa sababu kuu angalau mbili hivi.

Kwanza, wakati mamilioni ya Watanzania jana walikuwa wakiomba Jaji Tiganga atoe “no case to answer verdict” kuna genge la “wanaonufaika na kesi ya Mbowe” lililotamani maamuzi yawe kama hayo yaliyotangazwa jana, kuwa Mbowe na wenzake wana kesi ya kujimu. Sababu kuu ni ya kiuchumi. Kardi Mbowe na wenzie wanavyozidi kusota jela, ndivyo kadri watu hao wanavyonufaika kiuchumi kupitia kesi hiyo.

Unategemea “mtu aliyeletwa Dar kutoka kutoka mkoani kufanya coverage ya case” huku akilipiwa kila kitu atatamani “anasa hizo ziishe mapema” kwa Mbowe kurudi uraiani?

Lakini pili, kuna waliotamani sio tu Mama Samia asikutane na Lissu bali pia mkutano huo usizae matunda. Nililiongela hilo kwa kirefu kwenye makala hii

Barua Ya Chahali
Uchambuzi wa Kiintelijensia Kuhusu Mkutano Baina ya Mama Samia na Tundu Lissu Nchini Ubelgiji Hapo Jana
Jana, Februari 16 ya mwaka huu 2022, itaingia kwenye kumbukumbu za historia ya Tanzania baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, mjini Brussels, Ubelgiji, ambako Mama Samia yupo kwenye ziara ya kikazi…
Read more
3 months ago · Evarist Chahali

Takriban makundi yote mawili yana wahusika walewale, na good news kwao ni kwamba matakwa yao yanaelekea kutimia.

Wakati ili mkutano kati ya Lissu na Mama Samia uweze kuzaa matunda ni lazima wawili hao wawe “wadau wa mabadiliko husika” tayari kuna ishara kuwa “maafikiano hayo” yanaelekea kuvunjika.

Kwa sababu, kama nilivyotanabaisha pia kwenye makala hii ya kijasusi, Lissu ana kibarua kigumu cha kwa upande mmoja kuwa mshairika wa Mama Samia ili maombi yake ya chama chake yatimie na kwa upande mwingine aendelee kuwa mshirika wa “radical elements” ndani ya chama chake, ambazo anatambua kwamba zina uwezo wa kuhatarisha uhai wake wa kisiasa ndani ya chama hicho. Miongoni mwa radical elements hizo ni wanaharakati wa mtandaoni ambao kitambo sasa wanatazamwa kama ndio “walioshika rimoti” katika masuala mbalimbali kuhusu chama hicho.

Ndio maana hata kwenye “reaction” yake kuhusu uamuzi wa Jaji Tiganga, Lissu alikuwa “muted” kiasi, tofauti na huko nyuma ambapo angeelekeza mashambulizi moja kwa moja kwa Mama Samia. Katika twiti yake amewalaumu “majaji wa Magufuli na Samia.”

Twitter avatar for @TunduALissuTundu Antiphas Lissu @TunduALissu
Mwenyekiti Mbowe ana kesi ya kujibu ya ugaidi kwa mujibu wa majaji wa Magufuli na Samia, lakini ni 'Mwamba' na 'Rais' kwa mujibu wa wananchi wa kawaida wa Tanzania!!!

February 18th 2022

558 Retweets2,590 Likes

Ufumbuzi wa kesi ya Mbowe ukoje?

Kuna njia mbili tu. Moja ni hiyo wanayotaka Chadema, kwamba kumuomba Mama Samia aingilie kati ili kesi hiyo imalizwe “kibinadamu” ni suala ambalo kamwe halikubaliki.

Twitter avatar for @IAMartin_Martin Maranja Masese @IAMartin_
“No Retreat, No Surrender” Tunataka haki, sio huruma Kama itapatikana kwa Mbowe kujitetea sawa Kama itapatikana kwa DPP kuondoa kesi mahakamani sawa Lakini hatuwezi kupiga magoti kuomba msamaha Mtusamehe, kesho mtusimange kwa ugaidi? Hatupo tayari! Twende mbio ndefu tu

February 18th 2022

194 Retweets1,294 Likes

Na sio tu “hawataki suluhu na Mama SULUHU” bali pia wanaendelea kuwadhihaki ACT-Wazalendo kwa kukubali kushiriki kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.

Twitter avatar for @IAMartin_Martin Maranja Masese @IAMartin_
ACT wazalendo signed their deal with the devil (MaCCM) when they knew exactly what was to come. All they were interested in, was power. Othman Masoud even confirming it now, it’s hard dealing with CCM, within. Big zambarau backfire coming summer.. CCM ni hatari, shtukeni!

BBC News Swahili @bbcswahili

Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar asema hakuna hatua iliyofikiwa katika serikali ya umoja baada ya kifo cha Maalim Seif https://t.co/h0fjyhlBPJ

February 19th 2022

28 Retweets202 Likes

Kwa mwendo huu, ni dhahiri kuwa mkutano kati ya Lissu na Mama Samia sio tu hautozaa matunda kwa Lissu pekee hawezi kuwezesha “mwafaka” pasipo chama chake kuridhia, bali pia itamuwia vigumu Mama Samia kupatwa na utashi wa kuingilia suala hilo, kwa sababu “wenye kesi hawataki msaada wake.”

Njia ya pili ni hiyo ambayo “wenye busara” wamekuwa wakishauri kitambo, kwamba suala hilo limalizwe “kiutu” badala ya kisheria. Na njia pekee ya suala hilo kumalizwa kiutu ni kuhusika kwa Mama Samia, ambaye katika mamlaka yake anaweza kumuagisa DPP afute kesi hiyo kama alivyomuagiza afute kesi ya mashehe wa UAMSHO.

Kinyume na hili la pili, na sambamba na hilo la kwanza, ni kwamba kesi ya Mbowe iachwe mikononi mwa Jaji Tiganga. Lakini huhitaji kuwa na uelewa japo kiduchu wa sheria kubaini hukumu ya kesi hiyo itakuwaje.

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
CDM hawataki kusikia wazo la "msamaha wa Mama @SuluhuSamia" - ni haki yao kuwa na msimamo huo. Lakini wanafahamu fika hukumu ya Tiganga itakuwaje. Mashahidi wa utetezi wanaitwa kutimiza wajibu tu. Mpira upo mkononi mwao: kuafiki intervention ya Mama au kusubiri hukumu ya Tiganga

BABA IAN @mabelov3

@Chahali What is the end mr chalali ...kuna vitu huwa upo mbele plz nijulishe nijue tuu

February 18th 2022

2 Retweets14 Likes

Kabla ya kuchapisha makala hii nimekutana na hoja kwamba hatua inayofuata ya mashahidi wa Mbowe na wenzake kuanza utetezi wao “itafungua Pandora Box”,

Twitter avatar for @MabalaMakengezaRichard Mabala @MabalaMakengeza
Alipokamatwa nilisema walete kesi mahakamani haraka sana maana walidai wana 'ushahidi tosha' Baada ya huu 'ushahidi tosha' basi tusikie ushahidi upande wa pili. Wanadai tena ana kesi ya kujibu lkn wajihadhari. Kuwapa nafasi ya kujitetea kwaweza kufungua bonge la 'Pandora's Box

February 18th 2022

199 Retweets1,329 Likes

Yaleyale ya “kujipa matumaini kuwa ushahidi wa akina Kingai ni wa mchongo” lakini “ushahidi huohuo wa mchongo” ndio uliopelekea Jaji Tiganga aamue kuwa Mbowe na wenzie wana kesi ya kujibu.

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
Kama "ushahidi wa kimchongo wa akina Kingai" haujazuwia kumfanya Jaji Tiganga amkute Mbowe na wenzie wana kesi ya kujibu, I'm struggling to see how "kufunguka kwa Pandora Box" could make any difference. Mbowe alishahukumiwa alipokamatwa, kinachoendelea kortini ni formalities tu.

Richard Mabala @MabalaMakengeza

Alipokamatwa nilisema walete kesi mahakamani haraka sana maana walidai wana 'ushahidi tosha' Baada ya huu 'ushahidi tosha' basi tusikie ushahidi upande wa pili. Wanadai tena ana kesi ya kujibu lkn wajihadhari. Kuwapa nafasi ya kujitetea kwaweza kufungua bonge la 'Pandora's Box

February 19th 2022

1 Retweet

Lakini kuna hatari nyingine kubwa

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
"Pandora Box" indeed, kwa sababu kumekuwa na jitihada endelevu za sio tu kuwatambua mashahidi husika bali pia kuwafanya wawe "mashahidi wasio rafiki" - yaani ushahidi wao uusaidie zaidi upande wa mashtaka badala ya utetezi. Remember, Tanzania is a quasi-intelligence state.

Richard Mabala @MabalaMakengeza

Alipokamatwa nilisema walete kesi mahakamani haraka sana maana walidai wana 'ushahidi tosha' Baada ya huu 'ushahidi tosha' basi tusikie ushahidi upande wa pili. Wanadai tena ana kesi ya kujibu lkn wajihadhari. Kuwapa nafasi ya kujitetea kwaweza kufungua bonge la 'Pandora's Box

February 19th 2022

2 Retweets6 Likes

Miaka 60 ya uhuru wa Tanzania lakini kuna idadi kubwa tu ya Watanzania wasioelewa “how Tanzania works.” I just hope ni machale yangu tu ya kiasusi lakini as far as I know, kuna jitihada endelevu ya kuwafanya “mashahidi wautetezi wawakandamize washtakiwa badala ya kuwatetea.”

People’s Power iko wapi?

Jana, mbunge wa zamani wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema aliyepo ukimbizini nchini Canada, alitwiti kuhusu “umma” akimaanisha nguvu ya wanachama na wafuasi wa chama hicho.

Twitter avatar for @godbless_lemaGodbless E.J. Lema @godbless_lema
Umma huu ukiamua vyema ujinga na ukatili utasimama jana.
Image

February 18th 2022

194 Retweets2,143 Likes

Lakini huenda Lema amesahau kuwa ni umma huohuo unaompa matumaini ambao ulipoombwa na Tundu Lissu “uingie mtaani” Novemba mwaka 2020 baada ya hujuma ya kihistoria ya CCM kwenye uchaguzi mkuu, hakutokea mtu mmoja.

Ni katika mantiki hiyohiyo, maelfu ya wanaojazana kwenye “spesi” kila wiki wameishia kupiga porojo tu huku Mbowe na wenzake wakiendelea kuteseka huko jela.

Swali ambalo wana-Chadema wanakwepa kujiuliza ni kwamba je kuna tija yoyote kwa Mbowe kuendelea kuwa jela?

Hitimisho

Endapo Chadema wataendelea kusimamia kwenye “hatutaki msamaha” basi suala hilo litabaki mikononi mwa Jaji Tiganga. Na kila mtu mwenye akili timamu anafahamu hukumu itakuwaje.

Je Mbowe akikutwa na hatia - kwa ushahidi huohuo wa kimchongo, kwa sababu kimsingi “hukumu yake ilishaamuliwa alipokamatwa tu” - kisha Mama Samia akaamua kuingilia kati na kumwagiza DDP “afanye maamuzi ya kiutu”, Chadema wataendelea na msimamo wao kuwa “hatutaki msamaha”?

Kwa sababu hicho ndicho kinachotarajiwa kutokea huko mbeleni: Mbowe akutwe na hatia, ahukumiwe kifungo, kisha kilekile kilichokuwa kikipingwa kwa nguvu zote - msamaha wa Rais - ndio kimnusuru.

Ikumbukwe tu serikali haina tija kwa Mbowe kuwa huru. Lakini pia hata ikiamua kumwachia huru, inatambua bayana kuwa “baada ya kelele za siku mbili tatu, watu wataendelea na maisha yao.” Hao ndio Watanzania. Kama wameweza kustahimili machungu ya mgao wa umeme kwa zaidi ya miaka 20, watakoseshwa usingizi na serikali kumfunga au kumwachia Mbowe?

Wikiendi njema.

Share
Share this post
Free Access: What's next baada ya Mahakama Kuu kusema Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu?
www.baruayachahali.com
TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing