[Free Access] Machi 12 kama leo mwaka juzi nilitangaza kifo cha JPM...siku 5 zilizofuata zilikuwa balaa kwangu - nilitukanwa, nilitishwa, nililaaniwa...hadi serikali ilipothibitisha nilichotaarifu
Machi 12 kama leo, mwaka jana, nilitangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Kabla ya tangazo langu hilo, tayari kulikuwa na tetesi kadhaa kwamba afya ya kiongozi huyo ilikuwa tete.
Hata hivyo, kwa kupitia vyanzo vyangu vya kuaminika, nilikuwa mtu wa kwanza kutangaza kifo hicho. Lakini madhila yaliyonikumba baada ya kuweka taarifa hiyo hadharani, sintoyasahau.

Nilitukanwa, nililaaniwa, nilitishwa, na kwa hakika laiti hao waliokerwa wangeweza kunifikia, bila shaka muda huu ningekuwa marehemu. Lakini sio tu nilitangaza kifo hicho bali pia niliwafahamisha Watanzania kuhusu “ukweli” wa afya ya kiongozi huyo muda wote, huku watu mbalimbali “wakilishwa matango pori” kuwa yupo Nairobi, mara yupo India.


Hatimaye, siku tano baadaye, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo, Mama Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa kweli Magufuli amefariki.

Nami ikawa ahueni kwangu.
Baadhi ya walionitukana, walikuja kuniomba msamaha japo haikusaidia kitu. Hata hivyo nafarijika kwa kuwatumikia Watanzania wenzangu ipasavyo na kuendelea kuwa chanzo cha kuaminika cha habari mbalimbali.
Kusikiliza maelezo kamili kuhusu kilichojiri hasa siku hiyo hadi msiba ulipotangazwa rasmi, BONYEZA HAPA (dakika 8 tu)
Au sikiliza episode hiyo hapa Spotify
Jumapili njema.