Fahamu Hatua Tano/Saba Za MAJONZI, Zaweza Kusaidia Nyakati Hizi za #Coronavirus

Leo hapa Uingereza tumeanza "lockdown" ambapo sasa sio hiari kukaa ndani bali lazima.

Hatua hii haijawahi kamwe kuchukuliwa na nchi hii lakini "kuzuwia mikusanyiko na makutano (contact) yaonekana kuwa ndio njia yenye ufanisi zaidi kuzuwia kusambaa kwa maambukizi.

Twende kwenye mada. Wakati watawala huko wanaongea maneno matamu ya kuwapa watu matumaini, ukweli ni kuwa korona sio tu inaua bali inaua kwa kasi.

Kwa wastani, mgonjwa mmoja huambukiza watu watatu, jumla ya maambukizi yanakuwa watu wanne. Hao wanne wataambukiza watu sita zaidi, jumla inakuwa watu kumi, na kadhalika, na kadhalika.

Lakini jingine ni kwamba wenzetu huku hawaumi maneno. Wanatuambia kuwa tusipozingatia hatua kama hii "lockdown" tutaangamia kama inavyotokea Italia. Kuna tofauti kati ya kutishana na kuambiana ukweli.

Kwahiyo, tunakabiliwa na janga linaloweza kutuletea MAJONZI. Si kufiwa tu na tuwapendao bali pia kupoteza kazi, biashara kuanguka, nk.

Mada hii inahusu hatua za MAJONZI ambazo ukizifahamu zitakusaidia kuyakabili.

Kwenye picha hiyo hapo juu kuna michoro miwili. Mmoja una hatua tano mwingine una hatua saba. Kimsingi kuna hatua tano za MAJONZI ambazo waweza kuzipanua kuwa saba.

Tuanze na hizo tano. Hatua ya kwanza ni DENIAL yaani kukataa kuamini kama kilichotokea/kinachotokea ni kweli.

Hatua ya pili ni ANGER yaani hasira, yaweza kuwa dhidi ya "aliyesababisha" au dhidi yako mwenyewe.

Hatua ya tatu ni BARGAINING yaani kujaribu kutafuta "ufumbuzi hewa" kama vile kupania kulipa kisasi.

Hatua ya nne ni DEPRESSION yaani msongo wa mawazo.

Hatua ya tano ni ACCEPTANCE yaani "kukubali matokeo."

Kwenye mchoro wa pili wenye hatua saba, hatua ya kwanza ni SHOCK yaani mshtuko, na hatua ya sita ni TESTING yaani kabla ya kukubali matokeo, "unayatesti matokeo hayo" like "vipi kama ukweli ndio huu?" au "kwani kuna ubaya gani nikikubali matokeo?"

Si lazima upitie hatua zote hizo lakini kuzielewa kunaweza kukusaidia usikimbilie kufanya maamuzi mbaya.

Mada hii pia ipo kwenye blog yangu, link ipo kwenye bio yangu.

Take good care of yourself and others.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali