Explainer: Vita kati ya Russia na Ukraine…

Bandiko hili nililiweka huko Instagram jana. Kuna wadau wameomba nieleze kwa kifupi kuhusu Russia kuivamia Ukraine mapema leo. Kwa kifupi: What's happening? Russia hatimaye imeivamia Ukraine baada ya vitisho vilivyodumu kitambo Why? Putin, rais jasusi wa Russia, ametoa visingizio kadhaa. Kisingizio kikuu ni kwamba dhamira ya Ukraine kujiunga na Umoja wa Kujilinda wa Ulaya na Marekani (NATO) ni tishio kwa Russia. Pia amedai kuwa Ukraine imekuwa ikifanya mauaji ya kimbari (genocide) dhidi ya Waukraine wenye asili ya Russia.

Read →