DRC: Rais Tshisekedi alitarajiwa kuteua mkuu mpya wa idara ya ushushushu ya nchi hiyo, ANR, kufuatia kuugua kwa Mkurugenzi Mkuu Jean-Hervé Mbelu Biosha, kaimu wake Joseph Asumani atajwa kumrithi
Pia Gabriel Chadrack Boondo Lotika na Jean-Claude Bukasa watajwa kuwania nafasi hiyo
Rais Felix Tshisekedi huenda akalazimika kuteua mkuu mpya wa Idara ya Usalama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ANR, kufuatia kudhoofika kwa afya ya Mkuu wa Idara hiyo, Jean-Hervé Mbelu Biosha.
Mbelu Biosha ambaye aliteuliwa mnamo 2021 anaripotiwa kupelekwa Israel kwa matibabu ya dharura na nafasi yake ilitarajiwa kukabidhiwa kwa mtu mwingine.
Naibu wa…