Didier Abdallah Mlawa Na Mkakati Mkubwa Wa Kumchafua Mama Samia

Taarifa za kiintelijensia zinatanabaisha kuwa Didier Abdallah Mlawa, mmoja wa watu ambao wamekuwa mstari wa mbele kumtukana Rais wa Sita wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Saluhu, ameingizwa rasmi kwenye mkakati endelevu wa kumhujumu kiongozi huyo.

Awali mpango ulikuwa kuwa uchafuzi huo dhidi ya Mama Samia uanze mara tu baada ya kuisha kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Hata hivyo, changamoto za usafiri wa kimataifa kutokana na janga la Korona zimechelelewesha utekelezaji huo na sasa unatarajiwa kuanza mapema mwezi Juni.

Shambulio la kwanza linatajwa kumhusisha Mama Samia na mwanasiasa mmoja wa Zanzibar. Tayari kuna nyaraka mbalimbali ambazo wahusika wanapanga kuzitumia kama “ushahidi” kuhusu tuhuma hizo.

Inatarajiwa kuwa shambulio hilo litapelekea mtikisiko katika pande zote mbili za Muungano. Na jitihada za kuyumbisha Muungano zimeshaanza kwa kueneza uzushi kuwa “Mama Samia anaipendelea Zanzibar.” Mlawa pia amekuwa ajikaribu kujenga picha kuwa Mama Samia ni mdini.

Shambulio jingine linatajwa kumhusisha msanii mmoja maarufu wa kike wa bongo movie.

Wakati Mlawa atakuwa na “central role” ya kusambaza taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Twitter, akisaidiwa na akaunti zake kadhaa ambazo ni za bandia, na “washirika” wake nchini Kenya, kutafanyika pia jitihada ya kusambaza taarifa hizo kwenye magrupu ya Whatsapp na Facebook.

Mtumishi mmoja wa serikali ambaye alikuwa na nafasi muhimu wakati wa utawala wa marehemu Magufuli anatajwa kuwa licha ya kuwa miongoni mwa waasisi wa mkakati huo pia ametoa kiwango kikubwa cha fedha kufanikisha mkakati huo. Kabla ya kushika wadhifa huo muhimu, mtumishi huyo ambaye alihusika na masuala ya fedha kwenye kampeni za Magufuli mwaka 2015, alikuwa bosi wa taasisi moja ya umma inayomwagiwa fedha na wafadhili. Inafahamika pia kuwa mtumishi huyo alikuwa na undugu wa damu na marehemu Magufuli.

Mhusika mwingine ni mtumishi wa kitengo nyeti cha taasisi moja ya umma inayohusika na masuala ya mawasiliano. Dada huyo ambaye alikuwa na kazi maalum kwenye taasisi hiyo, aliyopewa na marehemu Magufuli, ambaye kama mtumishi aliyetajwa hapo juu, ana undugu wa damu na marehemu. Dada, huyo ambaye mumewe aliteuliwa na marehemu Magufuli kwenye taasisi muhimu ya kisheria, ni tajiri wa kupindukia, na hadi wakati makala hii inaandikwa alikuwa mbioni kutoroka nchi kwa sababu “takriban madhambi yake yote yako hadharani waziwazi” na anahofia kuwa huenda serikali ya Mama Samia itamchukulia hatua.

Wahusika wengine ni waandamizi katika wizara tatu muhimu, sambamba na baadhi ya watumishi waandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa wanaotoka Kanda ya Ziwa, na ambao zama za uhai wa marehemu Magufuli, walikuwa wakihusika na kiitwacho “kikosi kazi.”

Kadhalika, Bashite pia anatajwa kuwemo kwenye mpango huo japo taarifa mbadala zinaeleza kuwa kuna hofu kuwa Bashite “ana ukaribu na Mama Samia” na kwamba anweza kuwasiliti wenzie.

Mtu muhimu zaidi katika utekelezaji wa mpango huo ni Didier Abdallah Mlawa, kutokana na ushawishi wake mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, sambamba na msimamo wake mkali dhidi ya Mama Samia. Inaelezwa kuwa kwa kumtumia Mlawa, itakuwa vigumu kubainika kuwa “kuna watu nyuma yake.”

Ikumbukwe tu kuwa Didier Abdallah Mlawa ni “fugitive” aliyekimbia kifungo cha miaka 15 kwa kosa la wizi wa shilingi milioni 177, alichohukumiwa Agosti 2015. Baada ya kutoroka Tanzania, aliweka makazi yake nchini Kenya alikokuwa akitumiwa na “kitengo cha huko.” Miaka michache baadaye, watu hao walimsaidia mhalifu huyo kupaya viza ya kuja hapa Uingereza ambako aliomba ukimbizi kwa njia ya udanganyifu, na hadi sasa yupo hapa.

Taarifa zaidi kuhusu Didier Mlawa zipo kwenye MAKALA HII.