Dear Mama @SuluhuSamia, utu na busara itumike kumaliza mgogoro wa Ngorongoro
Kwa sie wenye uchungu wa dhati na Tanzania, twafahamu jinsi mafisadi wamkuwa wakijibidiisha miaka nenda miaka rudi kubaka raslimali za taifa letu. Miaka nenda miaka rudi, madini yetu yamekuwa yakitunisha akaunti za mafisadi kuliko kuwanufaisha walalahoi wa Kitanzania. Kadhalika, miaka nenda miaka rudi, mbuga zetu za wanyama zimegeuka kuwa zenye faida za…