Dear Mama @SuluhuSamia sie tunaokupenda kwa dhati na kukuombea ufanikiwe tunawajibika kukwambia ukweli huu, hata kama hautokupendeza
Dear Mama Samia,
Pole na majukumu. Pole pia kwa kuzushiwa taarifa kuhusu afya yako. Nitaongelea baadaye kuhusu hili la uzushi kuhusu afya za viongozi wetu.
Dear Mama, kilichonisukuma kukuandikia waraka huu ni vitu vitatu hivi vya msingi.
Cha kwanza ni matarajio ambayo mimi binafsi nimekuwa nayo tangu uingie mdarakani Machi 19, 2021. Matarajio hayo yalichan…