Dear Mama @SuluhuSamia, mabalozi hawa wawili wanakuhujumu
Inatanabaishwa kuwa moja ya dhambi kuu kwenye taaluma ya intelijensia ni kushindwa kutahadharisha. Hii inachangiwa na ukweli kwamba taaluma hiyo inatarajiwa zaidi kubaini matishio ya kiusalama kabla hayajasababisha madhara.
Makala hii ya kiintelijensia inaeleza kuhusu hujuma za mabalozi wawili wa Tanzania wanavyomhujumu Rais Samia Suluhu pamoja na Tanzania kwa ujumla.