Utangulizi
Jasusi amepokea maombi mengi kufuatilia utata uliotawala kwa zaidi ya wiki sasa kuhusu ajali ya Naibu Waziri mmoja, na wadau wengi kumtaka Jasusi afuatilie ukweli wa tukio hilo.
Lakini kana kwamba utata uliotawala ajali hiyo ya Mheshimiwa haukutosha, kumeibuka utata mwingine mkubwa kutokana na kifo cha binti mmoja ambaye kinahusishwa na tukio la awali.
Wakati yote haya yakitokea, ni wazi kuwa kuwa Rais Samia Suluhu anadhihakiwa kwa sababu laiti wanauhusisha na matukio hayo mawili wangehofia mamlaka ya uteuzi, wasingeendeleza maigizo ya kitoto yanayoendelea.
Makala hii itahitishwa kwa ushauri kwa Mama Samia kuhusiana na sakata hili.


