Dear Mama @SuluhuSamia, IGP Wambura anakuangusha, atoa vitisho kwa polisi waliohamishwa bila kulipwa senti tano ya uhamisho
Dear Mama Samia,
Pole na majukumu ya kulitumikia taifa letu. Kwa heshima na taadhima, naomba kukufikishia kilio cha askari kadhaa wa Jeshi la Polisi ambao wamehamishwa hivi karibuni lakini bila kupewa senti tano ya uhamisho.
Kwa upande mmoja, uhamisho huo wa ghafla na usio na posho za uhamisho umeziacha familia za maafande hao katika wakati mgumu kwa saba…